Kwanini uzinifu ni haramu? Ni sababu ipi na ni kwanini kitendo hiki, ambacho hakimdhuru yeyote, kiwe haramu?
Dear Brother / Sister,
Ikiwa jambo limefanywa kuwa haramu, ni haramu kwasababu Allah amelifanya kuwa haramu. Sababu zingine si halisi zenye kueleza kwanini ni haramu. Kwa mfano, nyama ya nguruwe ina madhara kwa afya ya mwanadamu na ni haramu kwasababu ya kuwa na virusi. Hata hivyo, hata kama madhara haya yataondolewa, itabaki kuwa haramu. Kuondosha madhara haikifanyi kitu fulani kuwa halali. Kwahiyo, madhara haya ni sehemu tu ya madhara ambayo tunaweza kuyaona. Kuna madhara mengi ambayo hatuwezi kuyaona na sababu ambazo zilikifanya kitu hicho kuwa haramu.
Kila kitu kilichoharamu kina madhara kwa mwanadamu. Hata hivyo, ni kwa kiasi gani tunazijua hizi haramu? Kwa kutokuzijua hakuzifanyi kutokuwa na madhara. Haikujulikana tangu zamani kwamba nyama ya nguruwe ilikuwa na madhara madhara yake yalionekana Dhahiri kutokana na maendeleo ya sayansi. Hivyo basi, watu wangaliipinga ikiwa madhara yake hayakuonekana zamani; sababu hiyo si sahihi. Tunapaswa kutii tuliyoamrishwa; kwa kadri sayansi inavyokuwa na faida za kumtii Allah hujitokeza, elimu yetu pia itaongezeka.
Sayansi bado haiwezi kufahamu hekima iliyopo nyuma ya maamrisho ya Allah; hujulikana kwa kadri muda unavyopita. Uzinifu una madhara mengi sana kwa mtu na jamii. Madhara yake yameelezwa na wanasaikolojia na wanasosholojia.
Uzinifu unazingatiwa kama haramu na kitendo kibaya sana katika Uislamu na dini zote za mbinguni zilizotangulia Uislamu. Ni moja kati ya madhambi makubwa. Adhabu yake ni kali kupita kiasi kwasababu ni uhalifu dhidi ya heshima ya mtu na kizazi/ukoo.
Maneno yafuatayo yameelezwa kwenye Kur’an:
“Wala msikaribie zinaa. Hakika hicho ni kitendo cha aibu na ni uovu.” (al-Isra, 17/32).
“Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara. Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka.” (al-Furqan, 25/68, 69).

Comments
Post a Comment