Kwanini dini zingine zisizokuwa Uislamu hazizingatiwi kuwa ni halali?
Allah, ambaye aliwatuma mitume na dini tofauti kwa wanaadamu katika enzi mbalimbali katika historia, aliuleta Uislamu uwe dini ya mwisho na Nabii Muhammad (s.a.w) awe mtume wa mwisho. Kwa kuja Uislamu, uhalali wa dini zilizotangulia kama Uyahudi na Ukristo ulifikia tamati.
Hiyo inalingana na hali ifuatayo: sheria mpya inapotungwa, iliyotangulia inakuwa haifai. Dini na sheria ya Allah ilipoletwa, uhalali wa dini na sheria zilizotangulia za Allah umefikia tamati.
Sababu kuu zinazolazimisha dini zingine zizingatiwe kuwa si halali ni kama ifuatavyo:
1- Awali ya yote, dini zilizotangulia ziliwahutubia watu mahususi wa enzi mahususi. Kwa upande mwingine, Uislamu unawahutubia watu wote. Ujumbe wake ni wa jumla na wa wote.
2- Dini zilizotangulia ziliwahutubia watu waliokuwa hai tu katika kipindi zilipoletwa. Sifa za watu waliokuwa wakiishi katika nyakati hizo zilikuwa za kifidhuli na tabia zao zilikuwa za kishenzi. Hawakuwa na maendeleo kwa upande wa sayansi, ustaarabu, fikra na ufahamu. Njia za usafiri na mawasiliano zilikuwa duni sana. Tamaduni, imani na desturi za kila sehemu na sehemu zilitofautiana. Kubadilishana fikra na tamaduni kulikuwa dhaifu sana.
Kwa hiyo, ikawa ni lazima kutuma mitume tofauti na dini tofauti kwenda katika sehemu tofauti. Muda ulivyosonga mbele na wanaadamu kupata maendeleo katika sayansi, fikra, utamaduni na ustaarabu, dini zilizotangulia za wenyeji zilibakia nyuma na zikashindwa kutimiza haja za watu. Kwa sababu hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukuka aliuleta Uislamu, dini ya mwisho, kwa wanaadamu.
Dini ya Uislamu ina rasilimali ya kuweza kumwambia kila mmoja, tokea watu wa miaka 1400 iliyopita, mpaka watu wa leo na watu wa baadaye. Kwa hiyo, uhalali wake ni wa kudumu na hautaisha mpaka Siku ya Kiama.
3- Muda ulivyozidi kusonga mbele, imani za kishirikina na potovu zilipenya na kuingia katika dini zilizotangulia. Kanuni ya kuamini u-moja wa Allah, yaani, imani ya tawhid, ilipotea. Uislamu bado unaendelea kuwepo huku ukiwa na upya wake na usafi bila ya badiliko lolote.
Kwa kuhitimisha, tunaweza kusema yafuatayo:
Dini zisizokuwa Uislamu ni kama taa za kandili zinazoangaza mtaa. Uislamu ni kama jua linaloangaza dunia nzima.
Je, kuna haja yoyote ya kuwepo taa ya mtaani linapochomoza jua?
Je, kufaa (uhalali) kwa taa ya mtaani kunaweza kuwepo pindi linapokuwepo jua?
Maswali juuyau islamu

Comments
Post a Comment