Kanuni zifuatayo ni muhimu ili soko huria lijitokeze wenyewe katika uchumi wa Kiislamu:
1- Lazima kutokufuja mali ya watu kwa dhuluma na kutonunua, na vitu viuzwe kwa kutumia mkataba wa kubadilishana na makubaliano ya kibiashara unaozingatia ridhaa ya pande mbili. Tumeshaeleza aya inayohusu jambo hilo hapo juu.
2- Kukataza riba na ulanguzi ni kanuni mojawapo iliyowekwa na Uislamu. Kama wanazuoni wa Kiislamu walivyosema, riba ni kitu cha ziada kisicho na ulinganifu. Bidhaa na pesa katika uchumi ni kama damu katika mwili wa binadamu; hivyo, ni lazima waendelee kuzungusha. Kwa hivyo, ulimbikizaji au kuweka mahali kama ziada itavimba kama saratani mwilini na kusababisha maradhi na mgogoro. Tumeshaandika aya inayohusu jambo hilo hapo juu.

Ulanguzi unamaanisha kuweka bidhaa ambazo watu wanazihitaji kwa kutarajia kupanda kwa bei zake. (Kamil Miras, Tajrid, VI, 448). Kuna hadithi kadhaa kuhusu jambo hilo. Kama vile, Muadh b. Jabal anasema: Nilimuuliza Mjumbe wa Allah kuhusu yaliyomo kwenye ulanguzi. Akasema, “Mtu hufurahi anaposikia kuwa bei iko chini na husikitika pindi bei zinapopanda. Ama kuhusu mlanguzi, huyo ni mtu mwovu; yeye husikitika kama Allah anashusha bei na hufurahi Anapozipandisha. (Haythami, Majmau’z Zawaid, IV, 101; Mansur Ali Nasif, at-Taj, Buyu, 2) Imesimuliwa kutoka kwa Mamar na Abu Hurayra kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Mtu anayeweka bidhaa kwa kutarajia kuwa bei zitapanda katika ardhi ya Kiislamu anatenda kosa.” (Haythami, ibid IV, 101 na at-Taj, Buyu, 2). Pia kuna hadithi zinazoeleza kuwa Allah atawatupia walanguzi Motoni. (angalia Haythami, ibid IV, 101)
2- Kukatazwa kupanga bei rasmi: katika uchumi wa Kiislamu, bei zilizopangwa, ukomo wa bei za juu na ukomo wa bei za chini usiwekwe. Ni haramu kupanga bei kwa mujibu wa rai ya wanazuoni wengi. Hata hivyo, imamu Malik anasema inaruhusiwa. Hata hivyo, lengo la kupanga bei ni kuzuia nguvu za mlanguzi anayezidisha bei katika soko kwa kuamua bei inayofaa. (Mansur Ali Nasif, Taj, II, 204, tanbihi: 4)
Mtume (s.a.w) hakuzingatia kuwa dola kupanga bei ndio njia ya kuzuia mfumuko wa bei. (angalia Fazlurrahman, İslamiyet ve İktiadi Adalet meselesi, (trans: Yusuf Ziya Kavakçı) s. 42). Ömer Nusuhi Bilmen anasema dola isipange bei na kuamua bei za bidhaa. Kuna hekima katika kila tendo la Allah. Kama ambavyo wakati mwingine bei hushuka na wakati mwingine hupanda kimaumbile, inatakiwa izingatiwe kuwa ni jambo la kawaida. (Ö.N.Bilmen, Istılahat-ı Fıkhiyye, VI, 125) Kwa upande mwingine, kupanga bei maalumu kunaweza kuwafanya watu wafiche bidhaa zao katika maisha ya kibiashara. Kuficha bidhaa husababisha bei zipande. Kupanda kwa bei kutawaumiza masikini. (Sayyid Sabiq, Fiqhu’s Sunnah, III, 105)
Imesimuliwa kutoka kwa Anas na Muhammad b. Abdurrahman kuwa mara moja bei zilipanda katika wakati wa uhai wa Mjumbe wa Allah (s.a.w). Watu wakamwendea Mtume na wakamwomba apange bei. Hapo, Mjumbe wa Allah akasema:
“Allah ndiye anayepanga bei, anasababisha wingi au uhaba na anatoa riziki. Ninaapa kwa Allah kuwa siwezi kukupeni wala kukuzuieni chochote kwa ruhusa yangu. Mimi ni mtunza hazina tu; ninafanya lile ninaloamrishwa kulifanya; Allah ndiye mtoaji. Ninataka kumfikia Allah bila ya kukiuka haki za yeyote kuhusu mali zao, maisha yao na damu.” (Abu Yusuf, Kitab-ul Kharaj, uk. 91; Abu Dawud, III, 272; Tirmidhi, III, 605; Ibn Majah, II, 741)
3- Mojawapo katika yaliyokatazwa katika uchumi wa Kiislamu ni kushindanisha bei za juu ili kuwaghilibu wanunuzi. Hilo husababisha mfumuko wa bei, na kuleta hali inayomnufaisha muuzaji na dhidi ya mnunuzi. Mtume (s.a.w) amewakataza watu kutokufanya najash. (Bukhari, III, 91; Ibn Majah, II, 733; Tajrid, VI, 457). Najash inamaanisha kujifanya mnunuzi na kupandisha juu bei ya kitu ingawa mtu huyo hataki kununua ili kuwahimiza wengine wakinunue na kuzidisha bei yake. (Marghinani, al-Hidaya, III, 40; Kasani, V, 233; Ibn Qudama, al-Mughni, IV, 160; Molla Khusraw, Durar, II, 177) Baadhi ya wanazuoni wanaizingatia najash, inayoleta faida haramu, kuwa ni makruhu kabisa (makruh tahrimi) (Muhammad b. Abdurrahman ad-Dimashqi, Rahmat-ul Ummah, II, 2); wengine wanaeleza kuwa si halali. (angalia Ibn-ul Humam, Fath-ul Qadir, V, 240)

4- Hakuna ushahidi katika Quran na Sunnah wa kupanga kiwango cha faida. Kwa hakika, kiwango cha faida kipo katika bei inayojitokeza mahali ambapo usambazaji na mahitaji hukutana. Haifai kwa mfumo unaotumia soko huria kupanga bei na kuweka kiwango cha faida. Kwa hivyo, hakuna tarakimu inayohusu faida katika aya na hadithi. Ni jambo la kawaida kwa bei kupanda kama mahitaji yataongezeka lakini isifikiriwe kuwa faida kubwa sana ni halali katika Uislamu. Kiwango cha kimaadili cha jamii, msawazo wa usambazaji na mahitaji, tofauti ya mahali na wakati na sababu nyingi nyingine huathiri kiwango cha faida. Baadhi ya wanazuoni wanasema faida ni katika kiwango cha nusu ya bei (Ö.N.Bilmen, Hukuku İslamiyye, VI, 120); baadhi ya wanazuoni wanataja kiwango cha 1/ 2 na 1/3 katika kupanga bei. (Angalia Celal, Yeniçeri, Yıllık, uk. 212) Pindi faida katika miamala ya murabaha ni kama kiasi cha mtaji, Abu Hanifa hazingatii kama inaruhusiwa kupata faida tena wakati wa kuiuza.
5- Katika hadithi hakuna upangaji kiwango cha faida lakini kuna mifano kadhaa inayotupa baadhi ya dhana kuhusu jambo hilo. Kama vile, Mtume (s.a.w) alipompa Hakim b. Hizam dinari 1 ili kumnunulia mnyama wa kumchinja sadaka. Hakim alinunua kondoo kwa dinari 1 na kisha akamuuza kwa dinari 2. Kisha, akamnunua kondoo mwingine kwa dinari 1 na akampa Mtume yule kondoo pamoja na ile dinari 1 nyingine. Mtume aliitoa ile dinari I kwa kuwapa maskini kama sadaqa na akamwombea dua Hakim awe na biashara nzuri. (Abu Dawud, III, 256; No: 3386) Tukio kama hilo lilifanyika baina ya Hz. Mtume na Urwa al-Bariqi. (Angalia Abu Dawud, III, 256; No: 3384) Katika hadithi zote mbili, tunaona kuwa kitu cha dinari 1 kiliuzwa kwa dinari 2 kwa faida ya asilimia mia moja. Maana yake, kwa faida iliyo sawa na mtaji.
Kuna hadithi nyingine kuhusu uhusiano baina ya mtaji na kiwango cha faida. Mtume (s.a.w) amesema, "Faida ya bidhaa ambazo hazikufidiwa na kufanyiwa kazi si halali. (Abu Dawud, III, 283, No: 3503; Ibn Majah, II, 737, No: 2187; Imamu Shafii, al-Umm, III, 70; Sarakhsi, Mabsut, XIV, 36). Maana ya faida ambayo haikufidiwa na kufanyiwa kazi huenda ikawa ni faida isiyo na urari wa faida-hasara, maana yake, isiyo na hatari. Sarakhsi (Sarakhsi, XV, 130–131; cf. Kasani, Badayi, IV, 206; Ibn-ul Humam, Fath-ul Qadir, V, 215, 265) anaeleza hilo kwa mfano ufuatao: mtu anakodi kitu kwa lira 100 na kisha anamkodisha rafiki yake au mtu mwingine bila ya kutumia gharama zozote au nyongeza yoyote kwa lira 120; hizi lira 20 ni faida ambayo hailipiwi au kufanyiwa kazi; yaani, haina hatari zozote. (angalia Kasani, IV, 206; Shawkani, Nayl-ul Awtar, V, 203 ff)
Kwa kuwa mtaji huwa na hatari zake na kama tutazingatia urari wa mtaji na hatari, tunaweza kusema chini ya nuru ya hadithi hapo juu na ijtihad ya Abu Hanifa kuwa kiwango cha faida mpaka kufikia kiasi cha mtaji kinaruhusiwa katika uchumi wa Kiislamu. Hata hivyo, hatumaanishi kuwa kuna kiwango na ukomo wa faida katika uchumi wa Kiislamu.
Kama tulivyoonesha hapo juu, faida ni kitu pamoja na shughuli kadhaa. Inaweza kuwa chini au juu kulingana na wakati, mahali na hali. Hata hivyo, kwa maoni yetu, kama faida imepatikana kutokana na kitu chini ya hali za kawaida ni zaidi ya mtaji wa kitu hicho, kiasi cha ziada, ambacho ni sehemu ya faida juu ya asilimia mia moja si halali.

6- Umuhimu mkubwa hupewa soko katika uchumi wa Kiislamu. Mtume (s.a.w) amesema yafuatayo kuhusu kutokuuza bidhaa njiani kabla ya kufika sokoni: “Msikatishe bidhaa za kibiashara katika njia ya kwenda sokoni…” Wanazuoni wa Kiislamu wamechunguza sababu za Mtume kukataza jambo la kukatisha bidhaa njiani na wakatoa maelezo kuhusu mmiliki wa bidhaa, wauzaji wa sokoni na watu wa eneo husika.
Huenda mwenye bidhaa akauza bidhaa zake kwa bei rahisi kabla hajafika sokoni kwa kuwa hajui bei na anaweza kupata hasara. Kwa hivyo, kama baadaye atafika sokoni, akaona kuwa bei ziko juu na kugundua kuwa ameghilibiwa, anaweza kutaka arejeshewe bidhaa zake na kutangua muamala. Wauzaji wa sokoni wasioweza kwenda nje ya mji ili kununua bidhaa kabla hazijafika sokoni watalazimika wanunue bidhaa hizo kutoka kwa wale waliozikatisha njiani; hivyo, watazinunua kwa bei ya juu na watapata hasara. Wale wanaozikatisha kabla ya kufika sokoni wataziuza kwa bei ya juu na watasababisha watu wa eneo hilo wapate hasara. Kwakuwa, kama wazalishaji wangefikisha bidhaa hizo sokoni, wangeziuza wenyewe moja kwa moja bila ya madalali na bei zisingekuwa za juu. (Imam Malik, Muwatta, IV, 307; Shafii, al-Umm, III, 93; Kasani, V, 232; Marghinani, IIı, 40; Ibn Taymiya, al-Hisba, uk. 11; Ibn Qayyim al-Jawziyya, at-Turuq-ul Hikamiyya, uk. 283; Ibn Humam, V, 239; M. Khusraw, II, 177; Ibn Nujaym, VI, 108; Shah Waliyyullah, Hujjatullah, II, 110; Sayyid Sabiq, Fiqh-us Sunnah, III, 11)

7- Kuna hadithi nyingine inayosaidia soko huria. Mtume amesema, “Watu wa mjini hawatakiwi kuuza bidhaa ya mwanakijiji kwa niaba yake.” (Bukhari, III, 94; Muslam, V, 17; Abu Dawud, III, 269) Basi, watu wa mjini wasiuze bidhaa za watu wa vijijini na wageni kwa niaba yao. Pindi Ibn Abbas alipoulizwa kuhusu maana ya hadithi hii, alieleza kama ifuatavyo: “Msijifanye madalali wao.”
Tunataka kutoa maelezo yafuatayo yanayotokana na Shafii: Wageni huleta bidhaa zao sokoni bila ya kulijua soko. Watu wanaoishi katika eneo hilo wanahitaji bidhaa. Hata hivyo, wenye bidhaa wanahangaika kupafikia mahali husika, kubeba bidhaa zao, n.k. Watu wanataka kuzinunua kwa sababu wanazihitaji. Kwa hivyo, wenyewe wanataka kuziuza haraka. Hivyo, bidhaa hizo zinauzwa baada ya kupatikana bei za soko, kwa bei inayofaa inayotegemea msawazo wa usambazaji na mahitaji. Kwa hivyo, wauzaji na wanunuzi wataridhika.
Kama tutachukulia kuwa watu wa mjini wanaziuza bidhaa hizo, madalali watazinunua kwa bei ya chini na kisha kungojea bei za soko zipande na kuziuza kwa faida ya juu. Hivyo, watawadhuru wenye bidhaa kwa kuwazuia kuziuza kwa bei inayofaa na watu wa eneo hilo kwa kulimbikiza bidhaa na kisha kuziuza kwa bei za juu. Kwa hali hiyo, pande zote mbili zitadhurika; kwa hivyo, Mtume amekataza mwamala wa namna hiyo. (Shafii, al-Umm, III, 92; Ibn Qudama, IV, 162; Ibn Qayyim, uk. 308)
8- Biashara mojawapo aliyokataza Mtume (s.a.w) ni kutaka kulipa bei ya juu kwa bidhaa ambayo mnunuzi na muuzaji wameshakubaliana kuuza na kununua. Mjumbe wa Allah amesema, “Msijaribu kununua kitu ambacho wawili wameshapatana. Ndugu yako anapotaka kununua kitu, usijaribu kukinunua kwa kulipa bei ya juu.” (Bukhari, III, 90; Muislamu, V, 12; Abu Dawud, III, 269)
Kwa mujibu wa hadithi hii, ni haram kuingilia biashara ya wawili waliokwishapatana na kuibatilisha. Ni haramu kumpa muuzaji bei ya juu kwa kitu ambacho amekubali kumuuzia mtu mwingine na kumwomba kuiacha biashara hiyo. (Marghinani, III, 90; Molla Khusraw, II, 177; Ibn Qudama, IV, 161; al-Ayni, Umdat-ul Qari, XI, 257; Ibn Humam, V, 239; Ibn Nujaym; al-Bahr, VI, 107; ash-Shawkani, V, 189)
9- Imekatazwa kuuza bidhaa kabla ya mtu kuzipata kwa sababu itasababisha bei nyingine mbali na inayotokana na bei ya soko. Mtume (s.a.w) amesema yafuatayo kuhusu jambo hilo: “Mnaponunua chakula, msikiuze kabla hamjakipokea.” (Ibn Majah, II, 749; No: 2226) Pia kuna maelezo yaliyosimuliwa kutoka kwa Ibn Umar. Wakati wa Mtume, watu walikuwa wakinunua nafaka kutoka kwa wafanyabiashara waliokuwa na misafara kabla hawajazipokea. Kisha, Mjumbe wa Allah akawatuma maafisa kwa wafanyabiashara. Aliwakataza kuuza nafaka kabla hawajazifikisha sokoni. Ibn Umar pia amesema kuwa Mtume alikataza kuuza nafaka zilizonunuliwa isipokuwa mpaka zikishapimwa na kupokewa. (Bukhari, III, 89; Muislamu, V, 23; No: 38; Nasai, VII, 287; Tajrid, VI, 437, No: 986) Ibn Umar aliongeza:
“Niliwaona baadhi ya walanguzi na walimbikizaji wakati wa Mtume. Walinunua chakula bila ya kupima na kupokea na wakataka kuwauzia wengine; walipigwa kabla hawajasafirisha bidhaa hizo na walikatazwa kuziuza bidhaa kabla hawajazipokea.” (Tajrid, VI, 446, No: 991) Hadithi hizi zilifafanuliwa kama ifuatavyo: kama mfanyabiashara anayeuza nafaka ataziuza kabla hazijafika sokoni, atasababisha bei zipande na kwa hivyo atawaumiza watu; kwa hivyo, ikakatazwa. (angalia Tajrid, VI, 437, Na: 986)

Mujazafa, maana yake, kuuza vitu bila ya kuvipima uzito na ukubwa, kwa maneno mengine, kununua vitu kwa jumla kwa mapatano, inazingatiwa kuwa ni halali. Hata hivyo, imekatazwa kuuza bidhaa zilizonunuliwa kama zile za kabla ya kuzipokea na kuzisafirisha kwa sababu ni namna ya biashara inayosababisha ulanguzi. Kama bidhaa zinazonunuliwa lakini hazijapokelewa zingeruhusiwa kuuzwa tena, basi baadhi ya bidhaa zilizowekwa ghalani zitapanda bei bila ya kutolewa na bila ulazima kwa kuuzwa tena na tena. Imeoneshwa na Ibn Umar kuwa inaelezwa katika hadithi kuwa ni lazima kupokea nafaka kabla ya kuziuza tena ili kuzuia kupanda kwa bei: Wenye bidhaa zinazofanyiwa mujazafa wanapigwa mpaka wazipakie nafaka hizo juu ya wanyama na kuzipeleka sokoni; inaelezwa kuwa kusafirisha bidhaa kutoka mahali zilipohifadhiwa kunamaanisha kuzipokea na kuzitoa, ambalo ndilo hitajio la Shari'ah ili kuzuia bei zisipande. Hili ndilo kusudio la hadithi. (Tajrid, VI, 447, 448)
9- Mtu asiyejiweza amekatazwa kununua na kuuza kwa sababu bei haitaendana na soko huria na itakuwa biashara iliyofanyika kwa sababu ya wajibu. Inaelezwa katika vyanzo kuwa aina hii ya kununua na kuuza, inayoitwa bay' al-muztar (kuuza au kununua ambako kumelazimishwa) ni haram. Inaelezwa katika hadithi iliyosimuliwa na Ali kuwa Mtume amemkataza mtu asiyejiweza kununua na kuuza. (Abu Dawud, Sharh Khattabi, III, 676)
Muuzaji anapouza bidhaa zake kwa mtu asiye na matumaini, atakiwa kumuuzia kwa bei ya kawaida bila ya kuzidisha; vinginevyo, ununuzi huu hautakuwa halali. (Ibn Abidin, IV, 110) Mtu anayepata kitu anachokihitaji tu katika sehemu moja, anahitaji kukinunua kwa bei ya kawaida. Muuzaji anatakiwa akiuze kwa bei ya kawaida hususani kama ni chakula au nguo ambazo mtu anapaswa kumuuzia. Ni wa wajibu kidini kwake kukiuza kama hivyo. (Ibn Taymiya, Fatawa, XXIX, 361)

Sasa, ninataka kunukuu baadhi ya kanuni kutoka katika kitabu changu, ambacho kilitayarishwa kama tasnifu ya udaktari, kinachoitwa “Kur'an-ı Kerim'e Göre İslam Ekonomisinin Esasları (kanuni za Uchumi wa Kiislamu Kwa mujibu wa Quran)”. Idadi kadhaa ya sura na aya zimewekwa katika mabano. Ni lazima kurejea katika sehemu inayoitwa Ushahidi na Maelezo ya nyenzo za kutafsiria aya.
Watu wameumbwa na kuelimishwa na Mola Mlezi mmoja. (2/139) Watu hawawezi kujiwekea wenyewe mfumo. Wanatakiwa kutafuta, wajifundishe na kutumia mfumo wa asili. (1/7) Mwanadamu ni chombo cha dola; kwa upande mwingine, ni kiumbe anayejitegemea anayeendeleza hadhi yake. (2/ 30) Hakuna anayeweza kunyimwa hadhi. (2/ 30) Mtu mmoja mmoja anaikabili dola moja kwa moja bila ya kutumia mshenga yeyote. (1/ 5)
Maisha ya kiuchumi ni maisha ya kimaumbile. Uingiliaji bandia katika maisha ya kiuchumi utayaharibu. (28/ 78) Lengo la shughuli zote za kiuchumi ni kuongeza idadi ya watu na bidhaa. (2/ 155) Maendeleo ya kiuchumi hupimwa kwa kiasi cha bidhaa na idadi ya watu. (9/ 69) Tabia ya kiuchumi hujiunda katika mfumo kutokana nao. Mwenendo mwema hautoshi; mfumo mzuri ni muhimu. (2/188) Akili ya kibinadamu inaweza kupata mfumo utakaotenganisha heri na shari, na bidhaa mbovu na bidhaa nzuri. (5/100) Ni wajibu wa dola kuweka mfumo. (1/1)
Uislamu una mfumo wa kiuchumi. (2/ 1–5). Biashara binafsi na biashara huria ni lazima katika Mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu. (2/ 286) Mifumo ya biashara binafsi na ushindani huria ni matokeo ya kimaumbile ya mabadiliko na uchaguzi wa kiuchumi. (3/ 140) Katika uchumi wa Kiislamu, dunia na ahera, maada na hali ya kiroho hupewa umuhimu unaolingana. Kimojawapo hakiwezi kutolewa mhanga kwa ajili ya kingine. (24/ 37) Hakuna amri inayokosekana katika Quran. (6/ 38) Mambo mengi yamesimuliwa kwa njia ya mfanano katika Quran. Jambo husimuliwa moja kwa moja au kupitia linalofanana nalo. (6/ 38) Mfumo wa Kiislamu haukubali riba. (2/ 278) Zakah-kodi ni kinyume cha riba. (2/ 280) Mfumo wa riba huria na mfumo wa zakah ni mifumo miwili inayopingana. (30/ 39) Baadhi ya sehemu za mfumo na amri haziwezi kutumika kwa kutenganishwa na sehemu zingine kuachwa; huzingatiwa zote kwa ukamilifu wake. (2/ 208)
Uzalishaji wa kimsingi ni mimea ya kijani inayohifadhi nguvu ya jua. (6/ 99) Uzalishaji wa kimsingi ni mazao ya ardhi. (6/ 99) Mfumo wa uzalishaji unategemea mzunguko wa maji yanayodondoka juu ya ardhi kutoka angani. (14/ 32) Mito inatoa mchango mkubwa katika uzalishaji. (14/ 32) Ardhi na mbingu, hewa na jua, udongo na maji vinashiriki pamoja katika uzalishaji. (14/ 32) Jua, mwezi, mchana na usiku ni nyenzo za uzalishaji; na huzalisha bure kwa ajili ya watu kimaumbile. (14/ 33) Uzalishaji na kwa hivyo utumiaji ni wa kijamii (wote). Kila mmoja anapaswa kutenda kulingana na hayo. (1/5) Vitendo vya uzalishaji, utumiaji na kubadilishana vitendo ni mambo ya kijamii. (2/ 274)
Dola ya Kiislamu haitofautishi baina ya raia Waislamu na wasio Waislamu kuhusu mambo ya kidunia. (3/110) Mali inamilikiwa na Allah; mtu mmoja mmoja ana haki na mamlaka ya kuitumia mali kwa niaba ya Allah. (2/ 180) Dola sio shirika la kijamii au la kibiashara lililoanzishwa na matajiri pekee; hivyo, masikini pia wanufaishwe na mapato ya dola. (59/ 7) Mapato yasiyo halali, bidhaa zilizofichwa na bidhaa haramu hayako chini ya dhamana ya dola. (2/ 270) Uvukaji mipaka katika mali binafsi unamaanisha kuvuka mipaka katika mali ya dola. Dola ina kazi ya kulinda mali zote. (3/ 26) Rais anaiwakilisha dola. (4/ 59) Wajibu wa mtu mmoja mmoja ni kuiweka serikali kwa kuitii. Haiwezekani kuongoza bila ya a serikali. (3/ 104) Serikali hutumia amri zinazoamuliwa kwa maafikiano. (4/ 59) Serikali hutunza na kuamuru na kufanya yaliyo mema. Serikali haziwezi kupanga bei. Hata hivyo, zinaweza kutaja bei zainazojileta zenyewe.. (3/ 104)

Serikali hazina haki na mamlaka ya kukusanya kodi ya ziada (2/ 272) kuongeza viwango vya kodi (3/ 161) na kuweka kodi mpya. (3/ 161) Mtu asiwaonee husuda wale wenye mali na wenye uwezo. (4/ 53) Mali na serikali hupewa wale wanaostahiki zaidi. (4/ 58).
Mirathi ni haki halali katika uchumi wa Kiislamu. (4/7) Mfumo wa mirathi uliowekwa na watu unatofautiana na mfumo anaoamrisha Allah. Mfumo wa mirathi wa Kiislamu una faida nyingi kwa upande wa uchumi. (4/ 11) Sababu za kurithi ni undugu, ndoa na ulezi. (4/ 8) Suala la kuchukua mtoto wa kupanga na kurithi kwa njia hiyo haiwezekani. Mtu hawezi kuteuliwa kuwa mrithi. (4/ 33) Mali ya mtu asiye na warithi hupelekwa hazina. (4/ 8)
Kufanya kazi kunamaanisha kushughulika kwa kusudio na kutumia nguvu. (2/ 204) Kazi ni uwezo na nguvu inayomfanya mwanadamu akimbie, afanye jambo na kusogea. Kazi ni manufaa na inamilikiwa na mfanyaji. Chanzo cha mali ni kazi. (53/ 39) Kazi si mali; kwa hivyo, mabadilikobadiliko ya usambazaji na mahitaji hayatumiki katika kazi ili kuendeleza urari wa mishahara kama ilivyo katika mali. (2/ 148) Wafanyakazi wa watu wanatofautiana. (92/ 4) Tofauti ya nguvu na uwezo baina ya watu huwezesha kubadilshana kazi (ajira) kutambuliwa. (43/ 32) Kazi, ni dhahiri kuwa kutakuwepo ugawaji kazi katika maisha ya kibiashara. (92/ 4) Viwango vya kazi zenye vigezo na zisizo na vigezo zinatofautiana. (6/ 132)

Mfuko wa kwanza katika biashara, mkopo na mambo mengine yanaitwa mtaji. (2/ 279) Katika Uchumi wa Kiislamu, mtaji una sheria mbalimbali; kwa hivyo, inawezekana kugawanya mtaji katika sehemu mbili ambazo ni mtaji wa kudumu na mtaji unaozunguka. (2/267) Si sahihi kutaka usawa wa watu kwenye mali na mtaji, kudai kuwa watu wako sawa na kuchukulia kuwa mtumwa na bwana wake wako sawa. (30/ 28) Zakah huweka mipaka ya juu kwenye mitaji; hivyo, ulimbikizaji uliokithiri wa mtaji umezuiwa na wenye mtaji wanashurutishwa kuwekeza. (2/ 276) Hakuna usawa wa ugawaji na uzuiaji mali katika jumuia. (3/ 35) Pindi mkopo unapotolewa kwa anayefanya kazi, hakutakuwa na utumiaji mbaya wa mtaji. (2/ 245) katika ubia wa mudharaba, mwenye mtaji hupata hasara. (2/ 267)
Bidhaa zinamaanisha kuwa Allah amewaumba watu ili wakidhi mahitaji yao duniani. (2/ 155) Bidhaa humwezesha mwanadamu kutimiza mahitaji yake, kukimu maisha yao, kudumu na kuwa ni mtawala duniani. Bidhaa ni vitu ambavyo maumbile ya mwanadamu yanavitaka na vinavyoweza kuhifadhiwa kwa ajili ya mahitaji ya baadaye. Kwa maneno mengine, bidhaa ni vitu vinavyoweza kununuliwa na kuuzwa, vyenye thamani na vinavyotaka kulipiwa na anayeviharibu. Kutokana na hayo, vitu kama mwangaza wa jua, nguvu ya jua na hewa vina manufaa sana lakini haviwezi kuzingatiwa kuwa ni bidhaa kwa sababu haviwezi kuhifadhiwa. Hata hivyo, gesi iliyojazwa kwenye mitungi huzingatiwa kuwa ni bidhaa kwa sababu imehifadhiwa. (4/5) Anachopata mwanadamu kwa kufanya kazi, anachokipata na kukitumia hitwa bidhaa. Kodi hutozwa juu ya vitu kama hivyo (kama vile, lami, petroli, mawe, metali zenye kuyeyuka na zisizo yeyuka, n.k) (2/ 272) Bidhaa ni za kimataifa na huzunguka baina ya mataifa. Ni lazima kuhakikisha mzunguko wa bidhaa na pesa baina ya matabaka yote. Bidhaa zina manufaa sana kwa wenye kuzihitaji zaidi. Kuna madhara pindi bidhaa na pesa zinapozunguka mikononi mwa matajiri tu. (59/ 7)
Haki ya mali kwa mtu inamaanisha kuwa na haki na mamlaka ya kumiliki bidhaa na vitu vinavyozingatiwa kuwa ni bidhaa na kuzitumia kwa uhuru kwa ajili ya manufaa yake mwenyewe. (3/ 26) Mali ni kitu cha muhimu na sifa ya kuwa binadamu. (9/ 34) Kila kitu ni kwa ajili ya mwanadamu; hakuna kiumbe mwingine mwenye haki ya kumiliki mali. (2/ 29) Mfumo wa mali ni mfumo wa dola nayo ni rehema kwa ajili ya watu. (4/ 29) Mfumo wa mali ni wa wajibu kwa mtu mmoja mmoja na jamii. Mtu mmoja mmoja anapaswa kutii mfumo wa mali madam anaishi katika jumuia. (2/ 180) Haki ya mali huwa chini ya mfumo wa kisheria. Kuiingilia mali ya mtu hairuhusiwi kamwe. Kupanga bei moja, kuweka fedha za kigeni na mikopo maalumu kamwe hakupo. Serikali haziwezi kuingilia kati uchumi isipokuwa kodi wanazotoza. (3/ 26) Mtu mmoja mmoja ana haki yenye mipaka yake katika mali. (3/ 26) Hakuna haki isiyo na mipaka katika mali bali yenye masharti katika uchumi wa Kiislamu. (24/ 33) Usawa katika mali na utumiaji si katika swali. (16/ 71) Si sahihi kutaka usawa kwa ajili ya watu kuhusu mali na mtaji. (30/ 28)
Katika mfumo wa uchumi wa Kiislamu, biashara binafsi na biashara huria ni lazima. (2/ 286) Kila mmoja anaweza kuchagua kazi yake mwenyewe na anajua kitu cha kuzalisha na namna ya kuzalisha. (2/ 148) Kazi hufanywa kwa kuzingatia mali binafsi na biashara binafsi, kwa pamoja na katika mfuatano. (2/ 110) Katika maisha ya kufanya kazi, mgawanyo wa kazi ni lazima. (17/ 84)
Mshahara ni malipo yatokanayo na kazi iliyotumiwa. Kodi ni malipo yatokanayo na kitu au huduma iliyotumiwa. (28/ 27) Ni halali kumwajiri mfanyakazi kwa ajili ya mshahara. (43/ 32) Urari baina ya faida na hasara, mshahara na kazi, kodi na mahali ni imara. Yanaunda urari baina ya hayo na mengine. (2/ 275) Mshahara hulipwa mfanyakazi sio kwa lengo la kumfanya aishi bali analipwa ili kufanya apate sehemu ya mtaji na kwa ajili ya kazi yake. (1/ 5) Mishahara hupangwa kwa kuzingatia uwezo wa kitaalamu, muda, elimu, uzoefu, uwezo na uchapakazi. (2/ 282) Mshahara hulipwa kama tu kilichofanyika kina manufaa. (65/ 6) Mtu asiyefanya kazi bila ya sababu yoyote hastahiki kulipwa mshahara. (6/ 158) Mkataba hauleti hakikisho la kupata mishahara; mishahara hulipwa baada ya kufanyika kazi. (65/ 6) Matumizi ya sheria zisizofaa za mishahara, mishahara ya kiasili na mfuko wa mishahara haifai. (28/ 27).
Faida hufidia hasara; ni kupanda kwa thamani ya bidhaa; ni tofauti ya bei. (2/ 275) Faida zinazopatikana bila ya hatari yoyote huzingatiwa kuwa ni riba. (2/ 275)
Kodi inamaanisha kuuza baadhi ya manufaa kwa ajili ya kupata pesa. Inaruhusiwa kukodisha mali na bidhaa zisizokwisha kama zitatumika kwa kiasi fulani cha pesa. Mfanyakazi anazingatiwa kujipangisha mwenyewe kwa kuuza kazi yake. Bidhaa zenye kwisha kama zitatumika haziwezi kukodishwa; kama vile, maji hayawezi kukodishwa, ng’ombe hawezi kukodishwa kwa ajili ya maziwa na mti kwa ajili ya matunda yake. Hizo sio bidhaa halisi; kwa hivyo, zinaweza kuuzwa tu. (28/ 27)
Riba inamaanisha kupata kitu kwa malipo ya kukopesha. (2/ 282) Riba ni kitu cha ziada kisichokuwa na chenye kulingana nayo. Riba huongezeka baada ya wakati fulani na kuwa mara mbili, mara tatu, n.k; riba imegawanyika katika sehemu mbili, fadhl (riba katika ziada) na nasia (riba juu ya mkopo). Riba ni haram kwa Waislamu wote. (3/ 130) Riba hupunguza uzalishaji, huzuia viwanda visifanye kazi na kuvisimamisha katika hatua fulani, na kusababisha migogoro. (30/ 39) Riba hupunguza ubadilishanaji bidhaa, huzuia mzunguko na hupunguza pato la taifa. (2/ 276) Wale wasiokubali kukatazwa riba huzingatiwa kuwa wameiasi dola ya Kiislamu. (2/ 279)
Mfumo wa riba hutafuna na kula pato la taifa. (2/ 275) Kwa kweli, pindi pato la taifa linapokua, mapato ya dola huongezeka, pia. (23/ 72) Kupata pesa kwa njia ambazo si halali na kuitumia kutapunguza pato la taifa. (5/ 42) Katika mfumo wa riba, pato la taifa litapungua; na katika mfumo wa zakah, pato la taifa litaongezeka. (30/ 39)
Katika mfumo wa uchumi wa Kiislamu, mmiliki wa mahali anapata kodi, mmiliki wa mtaji unaozunguka anapata faida na mfanyakazi anapata mishahara. (2/ 267) Ugawaji wa mapato umepangwa kiuadilifu katika jumuia. (2/ 134) Manufaa ya ziada yaliyopatikana kutokana na uzalishaji yanagawanywa katika kodi, mkopo, faida na mishahara inayotegemea shari'ah (mikataba). (3/ 73) Nchi zisizopanga ugavi wa mapato kwa uadilifu haziwezi kuendelea; zimegubikwa na hali ya kuanguka na kuporomoka punde. (2/ 134)
Nchi zinazoweka mfumo wao wa kimaumbile zitakuwa katika wingi na ustawi. (7/ 58) Wasiwasi na matatizo vinaondoshwa katika mfumo wa kiuchumi wa jumuia ambapo mfumo wa kodi umepangiliwa vyema; ustawi wa uchumi huondoa taabu na mashaka. (2/ 274) Heri na ustawi huhifadhiwa; hayo ni amani ya milele dhidi ya starehe za muda mfupi. (3/ 92) Mali na ustawi, umasikini na ubahili ni mambo ya kijamii. Maendeleo ya jumuia ni kwa ujumla wake. (2/ 155) Ustawi hutokea kutokana na vitendo vya kawaida vya kiuchumi. (5/ 66) Ustawi ni matokeo ya hatua ya kihistoria. (1/ 7) Baada ya jumuia kustawi, wingi na ustawi huongezeka. (7/ 95) Juhudi za mtu mmoja mmoja hazitoshi kwa ajili ya uokovu, ustawi na furaha; nyenendo za kijamii na vitendo ni muhimu. (3/ 186) Uhamaji husababisha wingi na mali. (4/ 100) Ndoa huleta wingi na mali, pia. (24/ 32) Nchi zisizoweza kuanzisha mfumo wa kimaumbile au wanauharibu hupata njaa na umasikini. (7/ 95) Ni lazima kupambanua baina ya heri na shari, bidhaa mbovu na nzuri, na bidhaa halali na haramu ili kuhakikisha ustawi. (5/ 100) Matendo machafu kama vile vilevi, kamari, masanamu na bahati nasibu yatakapoondoshwa kutoka mfumo wa kiuchumi, ustawi wa kiuchumi utaongezeka. (5/ 90) Jamii zinazochukua hatua za dhamana ya kijamii na kutoa haki za madaraja ya dhamana ya kijamii hupata ustawi. (30/ 38) Haiwezekani kuhakikisha ustawi na amani katika jamii kama masikini hawapewi bidhaa zinazofaa, chakula na nguo. (3/ 92) Kama mfumo wa biashara usio na riba ulioanzishwa na Uislamu utatumika kikamilifu, duniani kutakuwa mahali pa neema nyingi kama Peponi. Kuacha mfumo wa biashara usio na riba kutaleta mateso. (5/ 66) Jamii zinazoruhusu yaliyokatazwa na kukataza yaliyoruhusiwa haitaweza kupata ustawi na furaha. (16/ 116) Haiwezekani katika jumuia ambapo majirani hawasaidiani kuwa watapata ustawi na furaha. (107/ 1–7)
Matumizi kwa ajili ya starehe yanaitwa anasa. Inaruhusiwa kutumia bidhaa za anasa (bidhaa zinazotumika kwa ajili ya starehe si kwa sababu ni za lazima) chini ya masharti fulani. Anasa isimzuie mtu kutoa sadaka na kusaidia wengine, isimpe msukumo mtu kufanya mambo ya haramu kuhusu kupata pato, kutumia na kubadilishana, kusimpelekee ukosefu wa imani na hatari na isimzuie kuwa na imani na kutenda amali njema. (5/ 93)
Ubadhirifu unamaanisha kuvuka mipaka na kufanya mambo yaliyovuka mipaka juu ya jambo. (25/ 67) Katika hali yake ya ujumla, ubadhirifu unamaanisha kuchupa mipaka na kvuka wastani. Ubadhirifu unaweza kuwa katika njia mbili: kufanya mno jambo (ifrat) na kufanya jambo kidogo mno (tafrit). Maana yake, kufanya jambo kidogo mno pia ni ubadhirifu. (4/6) Anasa na matumizi ya kujionesha hakuzingatiwi kuwa ni mahitaji. Dola hailipii matumizi haya. (2/ 215) Jumuia ina mamlaka ya kuangalia kama bidhaa zinatumika katika njia ya ustawi au zinapotezwa ama laa. (6/ 141) Kutumia mali juu ya mapambo na uzuri kunaruhusiwa madam mtu hafanyi ubadhirifu. (7/ 32) Katika matumizi, kujionesha, anasa na matumizi ya kupoteza ni haram na ni dhambi lakini hayajakatazwa. (2/ 215) Waumini huepuka ubadhirifu na kujionesha katika matumizi. Wao hushindana kutoa sadaka sio kutumia ovyo na kujionesha. (3/ 14)
Vitu vya manufaa vinavyoufaa mwili vimefanywa halali na vinaruhusiwa; vitu visivyoufaa na vyenye kuudhuru mwili vimefanywa haramu na vimekatazwa. (2/ 175) Chakula chenye kuunufaisha mwili na kuweza kumeng’enywa ni halali na chakula kinachoudhuru mwili na hakiwezi kumeng’enywa si halali. (5/ 88) Allah Peke Yake Ndiye Mwenye haki ya kulifanya jambo liwe halali na haramu. Hakuna anayeweza kuamua kwa hiari yake mwenyewe kuwa kitu fulani ni halali au haramu. (2/ 275) Ni makosa kuzingatia kitu halali kuwa ni haramu. Inazingatiwa kuwa ni dhuluma na ukatili kukataza kitu ambacho ni halali. (5/ 87) Kilicho haram ni kutotumia bidhaa na kazi inapolazimu. (10/ 59)
Miamala inayozidisha matumizi ya ukingoni na kuweza kuwa na thamani kama bidhaa, kazi, pesa na mkopo kwa jumuia ni halali; na inayovipunguza hivyo ni haramu. Njia haramu za kupata pesa kama rushwa, kusema uongo, riba, kamari, wizi, matumizi mabaya, utapeli, upotoshaji, ghiliba, ulanguzi na kuchukua nafasi ya uchuuzi wa bidhaa kutoka kwa wamiliki wake kama gamba la mti linavyojibagua kutoka katika shina na kupunguza manufaa ya ukingoni. (5/ 42)
Katika uchumi wa Kiislamu, mfumo wa leo wa bima umebadilishwa kwa desturi ya infaq (sadaka). Katika uchumi wa Kiislamu, maisha ya kila mmoja yamedhaminiwa. Licha ya hivyo, hakuna desturi inayohakikisha malipo ya utoaji zawadi. Mfumo wa Kiislamu wenyewe ni bima. Hakuna kabisa haja ya kuwa na kampuni ya bima. Katika uchumi wa Kiislamu, ukusanyaji na ugavi kodi, maana yake, bajeti yenyewe inahakikisha maisha ya raia wote. Shukrani kwa ufahamu wa mali, taasisi na utawala wa Kiislamu, maisha ya wanyama wote na mimea yamedhaminiwa. Sababu ya infaq ni ndoa, ndugu na mali. Nafaqa inamaanisha kukidhi mahitaji ya chakula, vinywaji, nguo na makazi. (2/ 215) Dola ihakikishe mahitaji makuu ya kila mmoja. (6/ 164) Bima ya maradhi na ulemavu imechukuliwa na desturi ya ndugu katika Mfumo wa Kiislamu. (2/ 83) Nafaqa si msaada unaotolewa na ndugu bali ni matumizi ya fungu la dola katika faida ya mtu mmoja mmoja. (6/ 164) Mtoto huzaliwa, huishi na kufa katika familia na jumuia. (4/1) Pindi mtoto anapozaliwa, wajibu wa kumtunza ni wa baba kwa upande wa nafaqa (chakula). (65/ 6) Ndugu wasioruhusiwa kuoana au ndugu wanaoweza kurithiana wanatakiwa kutunzana. (17/ 26)
Siasa za kijamii au dhamana ya kijamii, elimu ya umma, mfumo wa kufanya kazi na kuishi yote hayo yamepangwa katika mfumo wa dola. (2/ 83) Msaada wa kifedha kwa ajili ya mtu hukusanywa katika familia kwanza, na kisha mtaani anapoishi, wilaya, mji, mkoa na kisha katika dola na duniani. (4/ 36) Ni muhimu mtu kutoa kitu bora zaidi ili awe mtu mwema kweli na kupata heri. (3/ 92) Bidhaa na wanyama wanaochinjwa huelekezwa katika jumuia ili kuhakikisha dhamana ya kijamii. (5/ 97) Dola inasaidia familia kadhaa pamoja na watoto wadogo, mtoto na mama. (6/ 151) Dola huwasaidia wenye matatizo ya kifedha na kulipa madeni yao. (2/ 280) Kila mmoja anapaswa kuwasaidia masikini kimwili na kutoa sehemu ya mali yake. (2/ 270) Licha ya wajibu wa kimwili unaotolewa kwa dola, ni muhimu kuanzisha taasisi za hisani kwa ajili ya misaada ya hiari. Taasisi za hisani ya kiuchumi zimeasisiwa pamoja na taasisi za hisani ya kijamii. (2/ 177)
Msaada wa kifedha kwa wazee, wagonjwa, watoto na masikini ni shukrani. (2/ 83) Hakuna anayeweza kuufuta baada ya kumsaidia mtu au kumfadhili. Sababu za wajibu wa kuwasaidia wengine mmoja mmoja ni kwa kuwa ni ndugu, kuishi jirani, kufanya kazi katika sehemu moja, ujirani na kutembeleana. (4/ 36) Wazazi, ndugu, yatima, masikini na wasafiri ndio ambao huweka urari wa kijamii. (2/ 215) Masikini hupewa haki zao kutoka Hazina. (17/ 26) Nchi zinazochukua hatua za hifadhi ya jamii hupata ustawi. (30/ 38)
Sadaqa (kodi) ni kodi ambayo walipa kodi hulipa kutoka katika mali zao kwa ajili ya Allah kwenda katika dola ili wapewe masikini. Sadaqa ni haki ya mafukara na masikini; si zawadi, sadaka au msaada. Sadaqa wanayopewa mafukara na masikini ni kama malipo na mishahara wanayopewa maafisa na wafanyakazi. Masikini ni yule ambaye pato lake la mwaka liko chini ya matumizi yake ya mwaka. Fakiri ni mtu asiye na mtaji na mwenye haki ya kupewa msaada kwa ajili ya kupata mtaji wake. (9/ 60) Masikini ni mtu asiyeweza kufanya kazi na fakiri ni mtu asiye na mali. Masikini hupewa pesa kutoka katika Hazina ili kukimu maisha yao na fakiri hupewa pesa kama mtaji. (2/ 83) Ndugu (dhul-qurba) ni watu wenye kushika nafasi ya kuwaangalia ndugu walio dhaifu majumbani mwao. Wenye kuwauguza wagonjwa na wazee wanazingatiwa kuwa wako katika kundi hili. (8/ 41) Ndugu, masikini, wasafiri na wengine hupewa haki zao moja kwa moja kutoka Hazina. (17/ 26)
Kuombaomba kunaangaliwa kuwa ni jambo baya. Hata hivyo, hilo linaruhusiwa kwa watu wasiojiweza wasio na kitu cha kuponea. Ni wajibu unaokaribiana na faradhi kuwasaidia waombaji masikini na wasiojiweza. Waombaji hawatakiwi kuumizwa au kuudhiwa; hata kama hakupewa kitu, hatakiwi kufukuzwa au kukaripiwa. Kama atang’ang’ania kuombaomba basi si masikini, anaweza kukaripiwa. (93/ 9-10)

Comments
Post a Comment