Je wanawake wamepuuzwa katika sheria ya Kiislamu?

Dear Brother / Sister,
Katika Uislamu, wanawake wamepata nafasi na thamani wanayostahiki na wamepata amani na furaha kamili waliyoitamani mara nyingi katika historia yote. Sheria ya Kiislamu imekomesha vitendo vya kukithirisha na kupuuzia na imeweka urari na utangamano baina ya jinsia mbili.
Kwa mujibu wa Uislamu, wanawake na wanaume wako sawa kwa upande wa kuwa w Mtume Muhammad anavyolieleza hilo, “Wanadamu wote wanaume au mwanamke wako sawa kama meno ya kitana.” (Bilmen, Ömer, Nasuhi, Hukuk-u İslâmiye ve İstilahat-ı Fıkhiye Kamusu, II. 73-74).
aja aliowaumba Allah. (al-Hujurat, 13; an-Nisa 1) Kama
Wanawake na wanaume ni nusu mbili za tufaha. Aya hii inalieleza hilo vizuri zaidi:
“Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao.” (Al-Baqarah, 2:187) Kama mavazi yanavyositiri sehemu za siri, kukukingeni dhidi ya joto na baridi, basi pia msitiriane na mrekebishane kasoro zenu.
Basi mjadala ‘kama wanaume au wanawake ndio walio bora’ haufai. Tena, kwa mujibu wa maelezo katika Qur’an, wanaume wana baadhi ya sifa na fadhila, wasizokuwa nazo wanawake; halikadhalika, wanawake wana baadhi ya sifa na fadhila wasizokuwa nazo wanaume. Kwa hiyo, jinsia zote mbili zinahitajiana katika sura mbalimbali; na kwa hivyo, jinsia zote mbili zina fadhila zinazotofautiana kimaumbile. Kulinganisha nukta zinazolingana kutatufanya tufikie kwenye majibu yasiyo sahihi. (An-Nisa, 4:34)
Kwa mujibu wa Quran, mwanadamu ana sifa moja tu pasi na kujalisha jinsia. Wanawake na wanaume wanawajibishwa kwenye sifa zinazolingana za kimaadili. Kinachozingatiwa mbele ya Allah ni maadili ya kidini na taqwa. Allah anatueleza ukweli huu katika Quran kama ifuatavyo:
Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi.” (al-Hujurat, 13)
Kama inavyoonekana, kwa mujibu wa Quran, kwa Allah undugu hautegemei jinsia, rangi au mbari ya mtu bali juu ya “maadili bora ya Kiislamu” yaliyoelezwa na Allah. Kiukweli, Allah anaeleza kuwa muumini mwanamume au mwanamke anayefuata maadili atalipwa mema duniani na ahera:
“Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.” (an-Nahl, 97)
Baada ya utangulizi huo mfupi, hebu tuangalie kwa ukaribu baadhi ya mila zilizofutwa na Uislamu kwa manufaa ya wanawake na haki ambazo Uislamu unawapa wanawake.
Baadhi ya Mila Zilizobatilishwa na Uislamu kwa manufaa ya Wanawake: Uislamu umekataa dhana kuwa wanawake wamelaaniwa, ambazo ni imani ya Wakristo na Wayahudi. Uislamu umekataza kwa nguvu desturi ya kuwazika watoto wa kike wakiwa hai, ambazo zilikuwa mila za enzi za kabla ya Uislamu Uarabuni. Mtume Muhammad (S.A.W) alitangaza kuwa hakukuwa na ndege mbaya katika chochote na kuvunja imani ya kuwaona wanawake kuwa ni nuksi. Aliwaamuru wanaume wawe na huruma sana, mapenzi na kuwajali wanawake. Aliitweza chuki dhidi ya watoto wa kike na akawasifu kwa kusema, “kuweni waadilifu wakati wa kuwapa zawadi watoto wenu; kama ningekuwa mwenye kupendelea, basi ningewapendelea watoto wa kike.” Katika kumjibu mmoja kati ya Masahaba zake aliyeuliza kuhusu nani alistahiki zaidi kuheshimiwa, alisema “Mama yako” mara tatu, katika mara ya nne alisema “Baba yako.”
2. Haki Zinazotambulika za Wanawake: Haki na wajibu ni maneno mawili pacha. Ikiwa kuna haki, lazima kuwe na wajibu pia. Sheria ya Kiislamu, ilitambua haki na uhuru wa wanawake kutoka mwanzoni kabisa na imetweza jambo la kuwadharau, umeweka majukumu juu yao. Kabla ya kuzitaja, tutakumbuka kanuni alizozitaja katika Hotuba ya Mwisho mbele ya watu 130.000:
“Enyi Watu! Ni kweli mnazo haki kwa wanawake wenu lakini nao pia wana haki juu yenu. Kumbukeni kuwa mmewachukua wawe wake zenu chini ya dhamana ya Allah na idhini yake tu. Kama watashikamana na haki zenu basi na wao wana haki ya kulishwa na kuvalishwa kwa ukarimu. Watendeeni wema na ukarimu kwani wao ni wenzenu na wasaidizi wenye kujitolea nafsi. Na pia ni haki yenu kuwa wasifanye urafiki na yeyote msiyemkubali, pia wasifanye machafu.
Katika hadithi nyingine, anasema tena, “Mcheni Allah kuhusu kutimiza haki za wanawake. Kuweni na hadhari ya kukiuka haki na uhuru wao. Kwani mmedhaminiwa hayo.” (Ajluni, Kashfu’l-Khafa, Beirut, 1351, I.36)
Baada ya majumui haya, hebu tuangalie kwa kifupi haki zinazotambuliwa za wanawake katika sheria ya Kiislamu:
Haki ya Masurufu (Nafaqa) kwa wanawake: Mume amewajibishwa kumpa masurufu mkewe na watoto aliomzalia. Yaani, wanawake wanaweza kudai masurufu kutoka kwa waume wao. Katika sheria ya Kiislamu, mume anatakiwa akidhi matumizi ya mkewe ya chakula, mavazi, makazi, na mtumishi. Wanawake wasishurutishwe kugawana uchangiaji matumizi: ni wajibu juu ya mume kuleta matumizi ya mke na watoto...
Haki ya wanawake ya kutenda: Katika sheria ya Kiislamu, wanawake wana haki ya kutenda. Wana uhuru juu ya mali zao wenyewe. Wanaweza kujipatia au kujichukulia wenyewe haki yoyote ya kiraia.
Zaidi ya hayo, uleaji watoto hupewa wanawake, kwa watoto wa kiume mpaka umri wa miaka saba, na kwa watoto wa kike mpaka waolewe.
Haki ya Mirathi: Kinyume na mifumo yote ya sheria za mila-desturia (isipokuwa Sheria za Kirumi) katika kipindi ulipoingia Uislamu, sheria ya Kiislamu ilitambua haki za wanawake katika mirathi. Desturi hii imezingatia usawa isipokuwa kwa kuwapa mafungu mawili makaka na fungu moja kwa madada miongoni mwa ndugu wa baba mmoja na mama mmoja. Mantiki ya desturi hiyo ya (fungu) moja kwa mawili imeelezwa kwa kiasi cha kutosha katika Qur’an na katika hadithi. Suala la wanawake kupunjwa katika mirathi si jambo la hakika.
Haki ya Kujifunza na Elimu kwa Wanawake: Kujifunza na elimu imekuwa na dhima kubwa katika jamii ya Kiislamu. Mwanamke ni mwalimu wa uhakika. Ni mwanamke ndiye kwa sehemu kubwa huwalea na kuwafundisha watoto. Haiingii akilini kuwa wanawake wanyimwe elimu. Mtume Muhammad (S.A.W) kila mara aliwahimiza na kuwaamrisha wanawake wajifunze kuandika na kusoma. Kulitokea idadi kubwa ya wanawake wasimulizi wa hadithi, wanafasihi wa kike, na la muhimu zaidi wanasheria wa kike katika historia ya Kiislamu.
Haki ya kufanya kazi: Wanawake wanaweza kuwa na taaluma yoyote, ambayo si kinyume na dini na maadili.
Haki nyingine ambazo Wanawake wanaweza kudai kutoka kwa Waume wao: Mwanamke anaweza kutaka mahari (mahr) yake anayostahiki kutoka kwa mumewe. Mbali na hayo, mume anatakiwa akae vyema na mkewe. Mwanamke anaweza kuzuru familia yake baada ya kumjulisha mumewe wakati wowote anapotaka kufanya hivyo. Mume ataniane na mkewe na kumruhusu kupata starehe za halali. Mume asimfanyie ukatili mkewe kwa sababu yoyote ile. Mume asifichue siri za mkewe.
Hebu tuoneshe kuwa ingawa wanawake wana haki hizo, mkuu wa familia ni mume. Hata hivyo, hiyo ni kanuni iliyochukuliwa kutoka katika mfumo wa sheria za Wayunani na Warumi. Kuafikiana na kanuni hizi hakumaanishi, kama wanavyodai baadhi ya wanasheria, kuwa zipo tofauti baina ya wanawake na wanaume. Aya inayoeleza ukweli huu kuwa mume ni mkuu wa familia pia inayakanusha madai hayo. Qur’an Tukufu inatangaza:
Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa.” (an-Nisa, 4:34)
Maswali juuyau islamu

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1