JE, NINASWALI VIPI? (KUSIMAMA, KURUKUU NA KUSUJUDU)

Mtu atasimama wima na kusema: (Allahu Akbar = Allah ni mkubwa sana). Atafanya hivyo huku akiwa amenyanyua mikono yake mpaka kwenye sehemu iliopo kati ya mabega yake na masikio yake.2
Ataweka mkono wake wa kulia juu ya wa kushoto, juu ya kifua chake. Atasoma suratul faatiha, na pamoja nayo atasoma Qur’ani itakayokuwa nyepesi kwake, ikiwa yupo katika rakaa ya kwanza au ya pili.
3
Atasoma Takbira huku akiwa amenyanyua mikono yake, halafu atainamisha mgongo wake kuelekea Kibla na kuweka mikono yake juu ya magoti yake. Na atasoma: (Sub-haana Rabbiyal-adhiim = Ametakasika Mola wangu Mtukufu) mara tatu.4
Atanyanyuka kutoka kwenye kurukuu na kusimama wima, huku akinyanyua mikono yake katika namna ya Takbira (ya kuanzia swala), na atasoma akiwa ni imamu au maamuma: (Samiallahu Liman-hamidah = Allah anamsikia anayemsifia). Wote baada ya hayo watasema: (Rabbanaa Walal-hamdu = Ewe Mola wenu, ni zako wewe tu sifa njema).
5
Atainama kwenda chini kwa ajili ya kusujudu huku akileta Takbira bila ya kunyanyua mikono yake. Atasujudu kwa kutumia viungo vyake saba: Paji la uso na pua, viganja miwili, magoti mawili na miguu miwili. Atasema mara tatu: (Sub-haana Rabbiyal-aalaa = ametakasika Mola wangu aliye juu zaidi). 6
Atakaa kati ya sijida mbili huku akiwa ameusimamisha unyayo wa mguu wake wa kulia, akiukalia mguu wa kushoto na kuiweka mikono yake juu ya sehemu ya mbele ya mapaja yake. Atasema: (Ewe Mola wangu, nisamehe na nipe rehema). Halafu atasujudu mara nyingine kama alivyofanya mwanzo.

(rakaa ya pili, tashahudi na Salamu)

7
Atanyanyuka kutoka katika kusujudu na kusimama wima kwa ajili ya rakaa ya pili. Katika rakaa hiyo ya pili, atafanya kama vile alivyofanya katika rakaa ya kwanza ikiwa ni pamoja na kusimama, kurukuu, kunyanyuka kutoka katika kurukuu, kusujudu.
8
Baada ya kusujudu mara ya pili kutoka kwenye kurukuu, atakaa kwa ajili ya Tashahudi ya Kwanza kama alivyo kaa kati ya sijida mbili, na atasema: «Attahiyyaatu Lillaah. Was-swalawaatu Wat-twayyibaat. Assalaamu alayka Ayyuhan-nabiyyu Warahmatullaahi Wabarakaatuh. Assalaamu Alaynaa Wa-alaa Ibaadillaahis-swaalihii. Ash-hadu Allaa Ilaaha Illallaahu Wa-ash-hadu Anna Muhammadan abduhuu Warasuuluh = Maamkizi ni ya allah na swala na mambo mema. Imani, rehema za Allah na baraka zake zikufikie ewe Mtume, na pia ziwafikie waja wa Allah walio wema. Ninakiri kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa ila Allah tu na ninakiri kuwa Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake). 9
Swala ikiwa ni ya rakaa tatu au nne, atasimama kwa ajili ya kuswali rakaa ya tatu. Atafanya katika rakaa hiyo ya tatu kama alivyofanya katika rakaa ya kwanza na ya pili, lakini hatasoma sura yoyote baada ya sura ya Alfaatiha. Vitendo na nyiradi za  kusoma  zilizo baki ni kama zile zilizo tangulia.
10
Katika rakaa ya mwisho, atakaa baada ya kusujudu na ataisoma Tashahudi ya Kwanza, halafu atamsalia Mtume. Namna ya kumsalia Mtume ni hii: (Allaahuma Swalli Alaa Muhammad Wa-alaa Aali Muhammad. Kamaa swallayta Alaa Ibraahiim Wa-alaa Aali Ibraahiim Innaka Hamiidun Majiid. Wabaarika Alaa Muhammad Wa-alaa Aali Muhammad Kamaa Baarakta Alaa Ibraahim Wa-alaa Aali Ibraahiim Innaka Hamiidun Majiid = Ewe Mola wangu, mrehemu Muhammad na familia ya Muhammad kama ulivyo mrehemu Ibrahimu na Familia ya Ibrahimu. Kwa yakini, wewe ni Msifiwa, Mtukufu. Na mbariki Muhammad na familia ya Muhammad kama ulivyo mbariki Ibrahimu na Familia ya Ibrahimu. Kwa yakini, wewe ni Msifiwa, Mtukufu).
11
Halafu atatoa salamu kwa kugeuka upande wa kulia huku akisema: (Assalaamu alaykum Warahmatullaah = Amani na rehema za Allah ziwe kwenu). Halafu atageuka upande wa kushoto huku akisema: (Assalaamu alaykum Warahmatullaah = Amani na rehema za Allah ziwe kwenu).

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU