IMANI YA MUISLAMU

Ujumbe wa Mitume wote kwa watu wao umeafikiana juu ya kumuabudu Allah pekee asiyekuwa na mshirika, na kuwakataa wale wanaobudiwa badala ya Allah. Hii ndio hakika ya maana ya Laa ilaaha Ilallah (hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah tu), Muhammad Rasuulullah (Muhammad ni Mjumbe wa Allah). Na hilo ndio neno ambalo kwalo mtu anaingia katika dini ya Allah. Shahada mbili: maana na masharti yake Kukiri kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah Nguzo sita za imani Kumuamini Allah Kuamini Malaika Kuamini Vitabu Kuamini Mitume Kuamini Siku ya Mwisho Kuamini Kadari

SHAHADA MBILI, MAANA NA MASHARTI YAKE

Ninakiri kuwa hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekee na Muhammad ni Mtume wake

Kukiri kuwa hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekee.

مآذن جامع الأزهر بالقاهرة

Nafasi ya tamko hili: Hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekee :

Uislamu umelipa tamko la Tauhidi Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah  tu nafasi kubwa sana na tukufu sana
  • Huo ni wajibu wa mwanzo kabisa wa Muislamu. Anayetaka kuingia katika Uislamu ni wajibu kwake kuliamini tamko hilo na kulitamka.
  • Na mwenye kulitamka akiliamini na, kwa kufanya hivyo, akimkusudia Allah   inakuwa sababu kwake ya kuokoka asiingie motoni, kama Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Kwa yakini, Allah ameharamisha kuingia motoni mtu ambaye ametamka: Hakuna mwenye haki ya kuabudia isipokuwa Allah tu kwa kufanya hivyo akiwa anamkusudia Allah  ». (Bukhariy, Hadithi Na. 415).
  • Na yeyote aliyekufa akiwa katika imani ya tamko hili atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, kama Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Yeyote aliyekufa na ilhali anajua kwamba hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah tu ataingia peponi». (Ahmad, Hadithi Na. 464).
Na kwa sababu hii, wajibu wa kujua maana ya Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah tu ni mkubwa sana na ni wa muhimu sana.

Maana ya «hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekee»:

Maana ni kwamba: Hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekee. Huko ni kuukana uungu kwa asiyekuwa Allah, na kuuthibitisha uungu wote kwa Allah pekee, asiye na mshirika.    
Muabudiwa ni kwa maana ya muabudiwa ambaye nyoyo zinamnyenyekea, zinamtukuza, zinamuogopa na kumtumaini. Yeyote anayekinyenyekea kitu chochote, akawa mtiifu kwenye kitu hicho, akakipenda na kukitumai atakuwa amekifanya Mola na muabudiwa. Vyote hivyo ni batili isipokuwa muabudiwa mmoja tu, naye ni Allah aliyetukuka.
Allah ndiye anayestahiki kuabudiwa pekee pasi ya vitu vingine visivyokuwa yeye. Yeye ndiye ambaye nyoyo zinamuabudu kwa kumpenda, kumtukuza, kumnyenyekea, kumtii, kumuogopa, kumtegemea na kumuomba.
 Haombwi msaada isipokuwa Allah pekee,hategemewi ila yeye tu, hakuna kuswali isipokuwa kwa ajili yake tu na hapachinjwi kwa kutaka kuwa karibu ila kwake tu. Ni wajibu kuifanya ibada iwe halisi kwa ajili yake yeye Mtukufu, kama alivyosema kuwa: «Na hawakuamrishwa isipokuwa tu wamuabudu Allah wakiifanya dini halisi kwa ajili yake tu». (Sura Albayyina, aya 4).
Na yeyote anayemuabudu Allah akiwa halisi kwake, akiitekeleza maana ya Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah pekee, atapata faraja kubwa, maisha maridhawa na mazuri. Nyoyo hazipati liwaziko la ukweli, utulivu na amani ya moyoni isipokuwa tu kwa kumuabudu Allah pekee, kama alivyosema kuwa: «Yeyote aliyefanya jambo jema, awe mwanaume au mwanamke na hali ya kuwa yeye ni muumini, kwa yakini kabisa, tutampa maisha mema». (Sura Annahli, aya 97).

Nguzo ya «hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekee»:

Tamko hili tukufu lina nguzo mbili. Ni lazima kuzijua ili maana na masharti yake yawe wazi:
Na hakuna vingine isipokuwa kwamba aina zote za ibada zinatikwa zifanywe kwa ajili ya Allah pekee, asiye na mshirika. Mwenye kufanya jambo katika ibada hizo kumfanyia asiyekuwa Allah atakuwa amemfanyia mshirika Allah.
Kama Allah alivyosema kuwa: «Na yeyote anayemuomba Mola mwengine pamoja na Allah  bila ya kuwa na ushahidi naye, hakuna vingine isipokuwa kwamba hesabu yake iko kwa Mola wake. Kwa yakini, ilivyo ni kwamba makafiri hawafaulu» (Sura Almuumnun, aya 117)
Na imekuja maana ya Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allah pekee katika kauli ya Allah isemayo kuwa: «basi yeyote aliyemkufuru twaqhut na akamuamini Allah, bila shaka ameshika kishiko madhubuti» (Sura Albaqara, aya 256).
Kauli yake kwamba «basi yeyote aliyemkufuru twaqhut» ndio maana ya nguzo ya kwanza (Hakuna muabudiwa wa haki), na kauli yake kwamba «na akamuamini Allah» ndio maana ya nguzo ya pili (isipokuwa Allah pekee).  

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU