Chinjo la kisheria

Chinjo la kisheria

Chinjo la kisheria ni kuchinja au kutoboa kulikotimiza shuruti zifuatazo:
  1. Mchinjaji awe Muislamu  au Mtu wa kitabu (Mkristo au Myahudi), aliyefikia umri wa balehe na awe amenuia kuchinja.
  2. Zana anayoitumia katika kuchinja iwe inafaa kuchinjia, inachirizisha damu kwa kukata, yenye makali kama vile kisu. Ni haramu kutumia zana ambayo itamuua mnyama kwa uzito wake au kugonga kichwa chake au kumuunguza kama vile kuua kwa umeme.
  3. Ataje jina la Allah (kwa kusema Bismillah) wakati anachinja.
  4. Kukata viungo ambavyo ni wajibu kuvikata katika kuchinja. Viungo hivyo ni hivi: Umio, koo na mishipa miwili mikubwa iliyopo shingono, au kukata viungo vitatu kati ya hivi vinne. 
    Masharti haya yakitimia, mnyama aliyechinjwa anakuwa halali kuliwa. Ama likikosekana sharti moja kati ya haya, mnyama aliyechinjwa anakuwa sio halali.

Aina za nyama katika migahawa na madukani

  1. Kuna mnyama aliyechinjwa na mtu ambaye sio Muislamu wala sio Mtu wa Kitabu, kama vile Budha, Wahindu na watu wasiokuwa na dini. Nyama hii ni haramu kula. Pia zinaingia katika uharamu nyama zinazopatikana katika migahawa na maduka yaliyopo katika miji ambayo wakazi wake wengi sio Waislamu na sio Watu wa Kitabu. Hukumu ya nyama hizo ni haramu mpaka ithibitike vinginevyo.
  2. Kuna mnyama aliyechinjwa na Muislamu au Mtu wa Kitabu kwa kufuata taratibu za kisheria. Nyama hii ni halali kula kwa mujibu wa matamshi ya Qur’ani.
  3. Kuna mnyama aliyechinjwa na Muislamu au Mtu wa Kitabu kwa taratibu ambazo sio za kisheria, kama kunyonga au kuzamisha kwenye maji. Nyama hii ni haramu bila ya mjadala wowote.
  4. Kuna mnyama aliyechinjwa na Mtu wa Kitabu na hakufahamika wakati wa kuchinja, na pia nyama inayopatikana katika migahawa na maduka yao. Msingi ni kwamba asili ya nyama hii ni kuwa inatokana na wanyama wao waliochinjwa kihalali na ni halali kula. Pamoja na hayo, ni vizuri kuweka umuhimu wa kutaja jina la Allah (Bismillahi) wakati wa kula, ingawa jambo bora zaidi ni kutafuta nyama halali ambazo uhalali wake uko wazi. 
Allah ametuhalalishia wanyama waliochinjwa na Wayahudi na Wakristo madamu hatujajua kuwa wamechinjwa kwa njia isiyokuwa ya kisheria kama kutumia umeme au kuzamisha majini. 

Uwindaji wa kisheria

Kuwinda wanyama na ndege ambao ni halali kuliwa, na ambao haiwezekani kuwakamata ili kuwachinja ni jambo la halali. Mfano ni aina za ndege ambao wapo misituni na vichakani na ambao hawali nyama. Pia swala, sungura na mfano wake. 
Katika kuwinda kuna masharti. Miongoni mwake ni haya:
  1. Muindaji awe na akili timamu, amekusudia kuwinda,  Muislamu au Mtu wa Kitabu. Sio halali kula mnyama aliyewindwa na Mpagani na mwendawazimu.
  2. Mnyama awe haiwezekani kuchinjwa kuotokana na hatari yake au ugumu wa kumkamata. Kama inawezekana kumchinja, kama vile kuku, mbuzu, kondoo na ng’ombe, haitakuwa halali kumuwinda. 
  3. Zana ya kuwindia iwe yenyewe inaua, kama vile mshale, risasi na mfano wake. Ama kutumia zana ambayo inaua kwa uzito wake, kama jiwe na mfano wake, basi haifai kula mnyama aliyewindwa kwa zana hiyo, isipokuwa tu kama atamuwahi  akiwa hai na kumchinja kabla hajafa. 
  4. Ataje jina la Allah kwa kusema: (Bismillahi) kabla ya kupitisha zana ya kuchinjia.
  5. Ikiwa mtu atamuwinda mnyama au ndege na kumkuta yuko hai baada ya kumuwinda, itakuwa wajibu kumchinja
  6. Ni haramu kumuwinda mnyama kama haikusudiwi kumla, kama vile mtu anayewinda mnyama kwa lengo la kujifurahisha na kujiburudisha, halafu asimle. 
Ni haramu kumuwinda mnyama kama haikusudiwi kumla, kama vile mtu anayewinda mnyama kwa lengo la kujifurahisha na kujiburudisha, halafu asimle. 

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU