Aya 6-18: Wewe Ni Mwendawazimu

Na walisema: “Ewe uliyeteremshiwa ukumbusho! Wewe ni mwen- dawazimu.
Waliosema ni maquraysh wakimwambia Muhammad aliyeteremshiwa Qur’an, kwa kumdharau. Kwa vile katika mantiki yao na vipimo vyao ni kwamba yeye ni mkichaa kwa kuwa anawaambia mambo yasiyowaingia; hata kama ni rehema kwa walimwengu na muujiza ulioshinda kwa elimu yake na mafunzo yake.
Mantiki haya hayahusiki na waabudu masanamu pekee yao wala wazandiki au walahidi; isipokuwa yanamkusanya kila anyeifanya dhati yake na manufaa yake ndio kipimo cha haki na mizani ya uadilifu, hata kama atasema: Lailaha illallah Muhammadur-rasulullah (Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu).
Kabisa! Hakuna tofauti baina ya Mwislamu huyu wa masilahi, ambaye amekubali utume wa Muhammad na mshirikina ambaye anapinga utume wa Muhammad; isipokuwa Mwislamu huyu amemwamini Muhammad kinadharia na akamakana kimatendo; na mshirikina amemkana kikauli na kimatendo. Kwa hiyo natija kwa upande wa kimatendo ni moja tu.
Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?
Hii ni kauli ya washirikina kwa Mtume (s.a.w.). Walitoa sharti la kuamini kwao kuwa Malaika wateremshwe kutoka mbinguni na washuhudie utume wa Muhammad, ndio akawajibu kwa kusema:
Hatuteremshi Malaika ila kwa haki na hapo hawatapewa muda.
Ufupisho wa jibu ni kuwa Mwenyezi Mungu huwateremsha Malaika kwa ajili ya kufikisha ujumbe na hawateremshi kwa waongo wenye inadi, isipokuwa kwa adhabu na maangamizi; kama alivyofanya kwa umma zilizopita. Lau kama Mwenyezi Mungu angeliwajibu washirikina kwa kuwateremshia Malaika, wangeliangamia wote. Umetangulia mfano wa Aya hii kwa swali na jawabu katika Juz. 7 (6:8).
Hakika sisi tumeuteremsha ukumbusho huu na hakika sisi ndio tuulindao.
Makusudio ya ukumbusho ni Qur’an. Imesemekana kuwa dhamir katika neno kulinda inamrudia Mtume kwamba yeye ndiye alindwaye kukingwa na maadui zake, lakini hilo ni kinyume na dhahiri ya Aya. Kwa hiyo inarudia kwenye ukumbusho ambao ni Qur’an, kama tulivyofasiri.
Unaweza kuuliza kuwa Mwenyezi Mungu anailinda na nini? Ikiwa ni kuilinda na kupotolewa, kama walivyosema wafasiri wengi, basi juzi juzi1 tu Israil ilichapisha maelfu ya nakala za Qur’an na wakaipotosha Aya hii: “Na mwenye kutaka dini isiyokuwa Uislam haitakubaliwa kwake” Juz. 3 (3:85), ambayo kwenye Qur’an ya Israil inasomeka hivi: “Na mwenye kutaka dini isiyokuwa Uislam itakubaliwa kwake.”
Na kama ukisema kuwa makusudio ni kuwa hakuna yeyote atakayeitia ila, itakuwa ni kinyume na hali halisi ilivyo. Sasa ni kulindwa vipi?
Razi na Tabrasi wameleta majibu mengi yasiyokinaisha. Tuonavyo sisi ni kuwa makusudio ya kulindwa Qur’an ni kuwa kila liliomo ndani yake ni haki inayothibiti kila wakati, isiyowezwa kupingwa wala kutiwa ila kwa hoja; bali kila akili na elimu zinaavyozidi kupanuka, hujitokeza dalili mpya za ukweli wa Qur’an na utukufu wake.
Maana haya ya kulindwa Qur’an tunayapata katika kauli yake Mwenyezi Mungu:
لَا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنْزِيلٌ مِنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ {42}
“Hautakifikia upotofu mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye hekima, Msifiwa” (41:42).
Na hakika tulikwisha watuma Mitume kabla yako katika mataifa ya mwanzo. Na hakuwajia Mtume ila walikuwa wakimfanyia istihzai.
Maneno haya anaambiwa Muhammad. Mataifa ya mwanzo ni umma uliokwishapita. Maana ni kuwa hali ya washirikina - kukukadhibisha wewe na kukuita kuwa ni mwendawazimu - ni kama hali ya washirikina wa zamani. Hakuwajia Mtume ila walimkadhibisha. Pamoja na hivyo walikuwa na subira na kuvumilia upumbavu wao. Lengo ni kumtuliza Mtume mtukufu (s.a.w.). Umepita mfano wake katika Juz. 7 (6:34).
Hivyo ndivyo tunavyouingiza katika nyoyo za wakosefu hawauamini na hali umewapitia mfano wa wa kwanza.
Dhamir ya tunavyouingiza na hawauamini inarudia kwenye ukumbusho (Qur’an). Maana ni kuwa Qur’an haiingii katika nyoyo za wakosefu kiukweli na kiimani; isipokuwa inaingia kidharau na kikejeli.
Kauli yake Mwenyezi Mungu ‘hawauamini’ ni tafsiri ya ‘tunavyouingiza.’ Maana ya ‘umepita mfano wa wa kwanza ni kuwa wakadhibishaji wa sasa ni kama wakadhibishaji wa zamani. Nyoyo zao zinaingia batili badala ya imani na upotevu badala ya uongofu.
Kusema kuwa Mungu anawaingiza ni kunasibisha kitu kwa sababu yake ya mbali moja kwa moja. Yamekwishapita maelezo ya hayo mara kadhaa.
Na lau tungeliwafungulia mlango wa mbingu wakawa wanapanda, baswangelisema“Machyetyamelevywabalsisnwatu waliorogwa.”
Katika Aya ilyotangulia, wapinzani walimtaka Muhammad (s.a.w.) kuwateremshia Malaika. Mwenyezi Mungu akwajibu kwamba Malaika hushuka na adhabu ya mangamizi kwa wapinzani na wakadhibishaji.
Kisha katika Aya hii akafuatishia jibu hilo kwa kusema kuwa lau atawafungulia milango ya mbinguni, kisha wapande kwa mili yao na wawaone Malaika na maajabu mengi, wangelisema: hakika Muhammad ameturoga na ametuonyesha njozi kuwa hali halisi na halisi kuwa njozi. Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:7).
Hakika tumeweka katika mbingu buruji na tumezipamba kwa wenye kuangalia.
Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa makusudio ya buruji ni nyota. Wengine wakasema ni vituo vya sayari ya Jua na Mwezi.
Vyovyote iwavyo, lengo la Aya sio kutufundisha elimu ya falaki ili tujue hiyo buruji hasa ni nini; isipokuwa lengo la kwanza kabisa ni kuzingatia na kutilia manani (tadabbur) uwezo wa Mwenyezi Mungu na hekima yake katika kuumba mbingu na ardhi na kwamba undani, nidhamu na uzuri aliouumba ni dalili wazi ya kuweko Mwenyezi Mungu na umoja wake, kuliko kuteremsha Malaika na kuliko miujiza yote wanayoitaka
Na tukazilinda na kila shetani afukuzwaye; isipokuwa asikilizaye kwa kuiba, naye hufuatwa na kijinga kinachoonekana.
Watu wa wakati wa jahilia walikuwa wakiamini kuwa kila kuhani ana shetani wake apandae mbinguni na kusikiliza mazungumzo ya Malaika kuhusu watu wa ardhini, kisha anashuka ardhini kwa kuhani wake kumpa habari. Aya mbili hizi zinapinga na kukana ngano hizi na kwamba mashetani hawawezi kabisa kupanda mbinguni. Na kusema kwake kijinga kinachoonekana ni fumbo la kuwa shetani hawezi kabisa hata kukurubia kuwasikilza Malaika; kama walivodai watu wa zama za jahiliya.
وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ شَيْءٍ مَوْزُونٍ {19}
Na ardhi tumeitandaza na tumeweka humo milima na tumeotesha kila kitu kwa wizani.
وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ وَمَنْ لَسْتُمْ لَهُ بِرَازِقِينَ {20}
Na tumejaalia humo maisha. Na ya ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.
وَإِنْ مِنْ شَيْءٍ إِلَّا عِنْدَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلَّا بِقَدَرٍ مَعْلُومٍ {21}
Na hakuna chochote ila hazina yake iko kwetu na wala hatukiteremshisipokuwa kwa kipimo maalum.
وَأَرْسَلْنَا الرِّيَاحَ لَوَاقِحَ فَأَنْزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَسْقَيْنَاكُمُوهُ وَمَا أَنْتُمْ لَهُ بِخَازِنِينَ {22}
Ntukazipelekpepza kupandishia na tukateremsha kutokmbingunmaji tukawanyweshhaywala nyinysimnaoyaweka akiba.
وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَنَحْنُ الْوَارِثُونَ {23}
Na hakika sisi ndio tunaohuyishntunaofishaNsisi ndio warithi.
وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنْكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَأْخِرِينَ {24}
Na hakika tunawajua watanguliao katika nyinyi na hakika tunawajua wachelewao.
وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ {25}
Na hakika Mola wako ndiye atakayewakusanyaHakika YeynMwenyhekima, Mjuzi.
  • 1. Kumbuka juzijuzi hiyo, ilikuwa ni katika mwaka wa 1969 - Mtarjumu.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1