Aya 19 -25: Na Ardhi Tumeitandaza

Na ardhi tumeitandaza na tumeweka humo milima na tumeotesha kila kitu kwa wizani.
Umetangulia ufafanuzi wake katika Juz. 13 (13:3).
Kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Kila kitu kwa wizani’ ina maana moja na kauli yake:
وَكُلُّ شَيْءٍ عِنْدَهُ بِمِقْدَارٍ {8}
“Na kila kitu kwake, ni kwa kipimo” Juz.13 (13:8),
Pia kauli yake:
وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا {2}
“Na akaumba kila kitu na akakikadiria kipimo” (25:2).
Yaani anachunga kiwango, aina, sura na lengo la kupatikana kitu hicho. Kama ingelikuwa ni sadfa basi kusingelikuwa na mpangilio huu.
Na tumejaalia humo maisha.
Yaani humo ardhini. Maana ya maisha ni zile sababu za maisha; kama vile kilimo, biashara na viwanda. Lakini maisha ya unyonyaji na uporaji hivyo ni viwanda vya shetani, sivyo alivyovijaalia Mwenyezi Mungu.
Na ya ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.
Kila kiumbe hai ardhini sisi hatukiruzuku wala hatukalifiwi na riziki yake, hilo liko wazi; isipokuwa lengo la ishara hii ni kuwa sisi tujue kuwa viumbe vyote hai vinaishi kwa riziki ya Mwenyezi Mungu, hakuna aliye hai anayeweza kumruzuku aliye hai; hata watoto tuwaleao na wanyama tuwafugao, riziki zao zote zinaatoka kwa Mungu, si kwa mwengine.
Na hakuna chochote ila hazina yake iko kwetu na wala hatukiteremshi isipokuwa kwa kipimo maalum.
Razi anasema: “Wameafikiana wafasiri kuwa makusudio ya chochote ni mvua, kwa vile hiyo ndiyo sababu ya riziki na maisha.” Lakini ukweli ni kuwa makusudio ya chochote ni mvua na mengineo. Kwa sababu neno chochote linaenea kwenye kila kitu; kama kusema sikumuona yeyote. Makusudo ya kuteremsha ni kutoa. Kiwango maalum ni sababu ya riziki. Maana ni kuwa heri yote iko kwa Mungu, Yeye ndiye anayewapa wenye kujitahidi, sio wavivu na wazembe. Mwenyezi Mungu ansema:
هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِنْ رِزْقِهِ ۖ {15}
 Yeye ndiye aliyewafanyia ardhi iwe laini basi nendeni katika pande zake na kuleni katika riziki zake” (67:15).
Kwa maelezo zaidi angalia kifungu ‘Je riziki ni bahati au majaaliwa?’ Juz.7 ( 5:100).
Na tukazipeleka pepo za kupandishia na tukateremsha kutoka mbinguni maji tukawanywesha hayo wala nyinyi sio mnaoyaweka akiba.
Pepo zimesifiwa kuwa za kupandishia mbegu kwa vile zinaabeba mawingu ya mvua na kufanya miti iwe inamea kutokana na mvua. Kwenye hali hii Mwenyezi Mungu ameishria mahali pengine kwa kusema: “Na yeye ndiye azipelekaye pepo kuwa ni bishara kabla ya kufika rehema yake. Hata zinapobeba mawingu mazito tunayasukuma kwa ajili ya mji uliokufa.” Juz. 8 (7:57).
Vilevile zimesifiwa kuwa ni za kupandishia kwa vile zinahamisha mbegu za maua ya kiume na kuzipeleka kwenye maua ya kike ili yaweze kutoa mazao na matunda.
Makusdio ya kusema: ‘wala nyinyi sio mnaoyaweka akiba’, sio kuwa maji yote yako kwenye tangi kubwa lililoko kwa Mwenyezi Mungu, hapana; isipokuwa makusudio ni kuwa Mwenyezi Mungu anayateremsha maji kwa sababu zake za kimaumbile, kuayahifadhi ardhini na kuyatoa kidogo kidogo, kupitia mito, kulingana na mahitaji.
Na hakika sisi ndio tunaohuyisha na tunaofisha. Na sisi ndio warithi.
Sisi ndio warithi ni fumbo la kuwa kila aliyeko ataondoka, hatabaki yoyote isipokuwa dhati ya Mola mwenye utukufu na kutukuka.
Na hakika tunawajua watanguliao katika nyinyi na hakika tunawajua wachelewao.
Razi na Tabrasi wametaja njia sita katika maana ya watanguliao na wachelewao. Usahihi ni kuwa makusudio ni kwamba hakifichiki kitu chochote mbele ya Mwenyezi Mungu katika hali ya waliotangulia na watakaokuja nyuma.
Na hakika Mola wako ndiye atakayewakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mjuzi.
Atawakusanya wote siku ya hisabu na malipo na ni Mwenye hekima katika kuwakusanya kwao huko, ambapo mtenda mema atapata thawabu za mema yake na mtenda maovu atapata adhabu ya movu yake. Vilievile Yeye anamjua aliyefanya mema na aliyefanya maovu.
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ صَلْصَالٍ مِنْ حَمَإٍ مَسْنُونٍ {26}
Na hakika tulimuumba mtu kutokanudongmkavu kwmatopmeusyenye kufinyangwa.
وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِنْ قَبْلُ مِنْ نَارِ السَّمُومِ {27}
Na majini tumewaumba kwa moto wenye joto kali.
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِنْ صَلْصَالٍ مِنْ حَمَإٍ مَسْنُونٍ {28}
Na Mola wako alipowaambia Malaika: “Hakika mimi nitamuumba mtu kutokana na udongo mkavu kwa matope meusi yenye kufinyangwa.
فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِنْ رُوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ {29}
Basi nitakapomkamilisha na nikampulizia rohyangu, basi muangukieni kumsujudia.
فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ {30}
WakasujudMalaikwote pamoja.
إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ أَنْ يَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ {31}
Isipokuwa Ibilisalikataa kuwa pamoja na waliosujudi.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1