Aya 120 – 124: Ibrahim Alikuwa Umma
Maana
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuashiria washirikina, katika Aya zilizotangulia, kwamba wao wamehalalisha haramu na kuharamisha halali, sasa anawatolea hoja kwa Ibrahim (a.s.) ambaye wanamtakasa na wanalazimisha kumfuata.
Mwenyezi Mungu amemsifu Ibrahim kwa sifa zifuatazo:
Mwenyezi Mungu amemsifu Ibrahim kwa sifa zifuatazo:
1. Hakika Ibrahim alikuwa ni umma. Wametofautiana katika kufasiri umma katika Aya hii. Razi amenukuu kauli nne, zenye nguvu zaidi ni kauli mbili: Kwanza kwamba Ibrahim alikuwa ni mwadilifu kwenye umma aliokuwa nao, Pili kwamba yeye alikuwa ni Imam. Vyovyote iwavyo ni kuwa makusudio ya umma hapa ni kuwa yeye alikuwa ni mkuu aliye adhimu.1
2. Mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu. Yaani mtiifu kwa Mungu.
3. Mnyoofu. Yaani mwenye kuachana na dini potofu, na kushikamana na haki.
4. Wala hakuwa katika washirikina. Hii ni kuwarudi washirikina ambao wanadai kuwa wao wako katika mila ya Ibrahim.
5. Mwenye kuzishukuru neema zake. Shukrani yake kwa Mwenyezi Mungu, kwa yale aliyomneemesha, alikuwa na ikhlasi.
6. Alimteua. Yaani alimchagua kuwa Mtume.
7. Na akamawongoza kwenye njia iliyonyooka, ambayo ni Uislamu sio Uyahudi wala Ukiristo:
مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَٰكِنْ كَانَ حَنِيفًا مُسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ {67}
“Ibrahimu hakuwa myahudi wala mnaswara (mkristo), lakini alikuwa Mwislamu, mnyoofu na hakuwa katika washirikina” Juz. 3 (3:67).
8. Na tukampa wema duniani ambao ni kuadhimishwa na watu wa dini zote na kukubali kuwa yeye ni Mtume
9. Na hakika Akhera yeye atakuwa miongoni mwa watu wema. Hii ni kuitikiwa dua yake pale alisema:
رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ {83}
“Mola wangu nitunukie hukumu na uniunganishe na watu wema” (26: 83)
Kisha tukakupa wahyi kwamba ufuate mila ya Ibrahim mnyoofu na hakuwa katika washirikina.
Hii ni dalili kwamba Uislamu na dini ya Ibrahim ni moja katika itikadi na kuukana ushirikina. Basi mwenye kudai kuwa yuko katika dini ya Ibrahim na huku anaukana utume wa Muhammad atakuwa amejipinga yeye mweyewe, atake asitake.
Unaweza kuuliza kuwa Muhammad (s.a.w.) ni bwana wa Mitume, itakuwaje aamrishwe kumfuata Mtume mwengine?
Jibu: Lengo la kufuata hapa ni kuwarudi washirikina amabao wanaikubali dini ya Ibrahim na kuipinga dini ya Muhammad (s.a.w.) na hali ni kitu kimoja. Zaidi ya hayo ni kuwa amri ya kufuata hapa ni kwa kutangulia; yaani amfuate aliyemtangulia. Na kutangulia hakumaanishi ubora zaidi katika jamabo lolote.
Hakika Sabato iliwekwa kwa wale waliohitalifiana tu kwenye hiyo.
Makusudio ya kuwekwa ni kuwa ni wajibu; yaani Mwenyezi Mungu alilazimisha kuadhimishwa sabato (Jumamosi) na kuacha kufanyakazi kwa mayahudi peke yao wala haikuwekewa yeyote kabla yao wala baada yao.
Inasemekana kuwa jamaa miongoni mwao waliikataa Ijumaa; wakawa hawataki siku nyigine isipokuwa Jummamosi tu. Ndipo Mwenyezi Mungu akawakubalia, lakini kwa sharti la kuwa wasivue siku hiyo. Basi wakakubali sharti, lakini hawakulitekeleza; kama ilivyo desturi ya mayahudi siku zote na sehemu zote.
Mwenyezi Mungu hakubainisha sababu ya kutofautiana katika Sabato, kuwa je, walitofautiana katika ruhusa ya kufanya kazi siku hiyo, au walitofautiana kuhusu Sabato yenyewe kwamba wengine walisema ni sikukuu na wengine wakasema si sikuu?
Lililo na nguvu ni kuwa wao waliotofautiana katika uharamu wa kuvua siku hiyo; kama tulivyodokeza katika Juz.9 (7:163 – 166). Kwa sababu wote waliafikiana kuwa sabato ni sikukuu.
Na hakika Mola wako bila shaka atahukumu katika lile walilohitalifiana siku ya Kiyama.
Na hukumu yake siku hiyo itakuwa ni kuwapa thawabu watiifu na kuwaadhibu waasi.
ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُمْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنْ ضَلَّ عَنْ سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ {125}
Waite kwenye njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako ndiye anayemjua zaidi aliyepotea njia yake na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.
وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُمْ بِهِ ۖ وَلَئِنْ صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِلصَّابِرِينَ {126}
Na kama mkilipiza basi lipizeni kama mlivyofanyiwa. Na kama mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanaosubiri.
وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِاللَّهِ ۚ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُ فِي ضَيْقٍ مِمَّا يَمْكُرُونَ {127}
Na subiri na subira yako haikuwa ila kwa Mwenyezi Mungu, wala usihuzunike wala usiwe katika dhiki kwa hila wanazozifanya.
إِنَّ اللَّهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوْا وَالَّذِينَ هُمْ مُحْسِنُونَ {128}
Na wale ambao wanatenda mema Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kucha.
- 1. Mwenye tafsir Rawhil bayan alipofasiri Aya hii, alisema: “Imeelezwa katika Hadith ‘Hassein ni mjukuu katika vitukuu” yaani umma katika ummati. Kwa maana ya kuwa vitukuu ambao ni masharifu wanatokana na kizazi cha Zaynul’abidin, mtoto wa Husseni. Kwa hiyo ameeneza umma. Kisha akaendelea kusema mwenye Rawhil-bayan: “Baadhi ya jamaa wakati wake walisema kuwa Hussein ni mtume”. Na sisi hatujawahi kusikia hili. Hakuna shaka kwamba hilo ni ukafiri na ulahidi.

Comments
Post a Comment