Vituko vya Bibi Fisi: Mchawi aliyetikisa Kanda ya Ziwa Mpaka Serikali Kupindisha Barabara Kumpisha


Kuanzia katikati ya miaka ya sitini hadi mwishoni mwa miaka ya tisini katika mji Mwanza aliishi kigagula mmoja ambae alijulikana kwa jina la Bibi Fisi.
Loading...

Bibi Fisi alikuwa mchawi hatari sana ambae sifa zake zilitikisa mkoa wote wa Mwanza na.mikoa jirani ya kanda ya ziwa..

Kigagula huyu inasemekana alikuwa na nguvu kubwa sana za kichawi na inasemekana kuwa alikuwa mmoja kati ya wachawi waliokuwa katika ranks za juu kabisa katika ufalme wa kichawi wenye makao yake makuu katika mkoa wa Shinyanga ( now Bariadi) katika eneo ambalo linajulikana kama Gamboshi ( ile isiyo onekana )

Pia inadaiwa kwa nguvu na uwezo wake mkubwa katika fani ya uchawi hakukuwa na mchawi yoyote nchini Tanzania ambae alikuwa na uwezo kama wa kwake.

Chanzo cha Bibi huyu kuitwa Bibi Fisi ni kwamba alikuwa ana kibanda ( nyumba ) yake katika eneo la Bugando jijini Mwanza.. Kibanda cha bibi huyu kilikuwa pembeni ya barabara.

Serikali ya Mwl Julius Kambarage Nyerere ilitaka kupanua barabara na moja kati ya nyumba ambazo zilitakiwa kubomolewa ni pamoja na nyumba yake.

Bibi huyu aligoma kuondoka katika kibanda chake kupisha upanuzi wa barabara..

Watu wa Halmashauri ya mji wa Mwanza hawakuwa na jinsi zaidi ya kufanya maamuzi ya kuvunja nyumba yake ..

Licha ya sifa za kutisha za bibi huyu lakini watu wa Halmashauri ya mji wa Mwanza walifikia uamuzi mgumu wa kuvunja nyumba ya bibi Fisi kwa kuhofia kuwajibishwa na mwalimu ( Viongozi wa Halmashauri mnaanzaje kuwambia Mwalimu kwamba kuna bibi kizee amegoma nyumba yake kuvunjwa na sisi tumeshindwa kutumia nguvu kwa sababu tunaogopa anaweza kuturoga )

Hakuna dereva aliye kuwa tayari kuendesha Grader ili kuvunja nyumba ya Bibi Fisi..Kila dereva aliyefuatwa aligoma ..

Watu wa Halmashauri wakafikia muafaka wawatumie wafungwa walio kuwa wamehukumiwa kunyongwa ambao walikuwa wanasubiria adhabu yao katika gereza la Butimba lililopo kusini mwa jiji la Mwanza..

SIKU YA KUVUNJA NYUMBA YA BIBI FISI

Inasimuliwa kwamba madereva walipoenda kuvunja nyumba ya bibi huyo nyumba ilitoweka na kitokea Fisi wengi sana katika eneo hilo hali iliyozua taharuki kubwa kwa wakazi wa maeneo ya Bugando,Bugarika,Igogo na mji wote wa Mwanza kwa ujumla.

Wengine wanasema Bibi huyu aliitwa Bibi Fisi kwa sababu alikuwa anafuga Fisi kwa ajili ya shughuli zake za ulozi na uchawi.

Tukio hili la bibi Fisi liliwatisha sana viongozi wa mji wa Mwanza ambao waliamua kumtaarifu Mwalimu.

Inasemekana Mwalimu alienda hadi nyumbani Kwa bibi huyu kwa ajili ya kuongea NAE na kumsihi akubali kupisha upanuzi wa barabara katika eneo hilo na kwamba serikali itamjengea nyumba nyingine nzuri katika eneo ambalo bibi huyo atalichagua mwenyewe lakini bibi Fisi alikataa kata kata kwa madai kwamba lile ni eneo ambalo amerithi Kwa mabibi na mababu zake na kwamba makaburi ya mabibi na mababu zake wote yapo katika eneo hilo na kwamba hawezi kuwakosea heshima wazee wake kwa kuliacha eneo hilo..

Mwalimu Nyerere kwa kuwa aliheshimu sana imani za watu hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na bibi huyo..

Hatimae upanuzi wa barabara ukampisha yeye na sio yeye kupisha upanuzi wa barabara.

Bibi huyu inasemekana alikuwa na utajiri mkubwa sana ambao hata hivyo ulikuwa hauonekani kwa macho ya nyama .

Chanzo cha utajiri wake inasemekana ilikuwa ni misukule.

Bibi huyu alikuwa anawauza misukule wake kwa wafanyabiashara wakubwa wa kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla.

Wateja wake wakuu inasemekana walikuwa wafanya biashara wa kihindi.

Watu wengi waliogopa kupita peke yao karibu na nyumbani kwa bibi huyu na ilikuwa ikifika usiku basi watu walikuwa hawapiti kabisa katika eneo hilo..

Inasemekana pia ilikuwa ukiingia kwenye kibanda chake unakutana na mjengo mmoja wa hatari sana .

Karibu na nyumbani kwake bibi huyu alikuwa na shamba la kama robo heka ambalo lilikuwa na mazao karibu wakati wote wa mwaka..

Bibi huyu alikuwa na maajabu sana. Mwaka 1983 kuna watoto walikuwa wakisoma katika shule ya msingi Mlimani ambayo haipo mbali sana na mahali ilipo nyumba ya bibi Fisi

..Watoto hao wa shule wakati wakati wanarudi makwao walipita nyumbani kwa bibi Fisi na kwenda kuiba maembe kwenye mti wa maembe ulio kuwa katika shamba la bibi huyo.

Bibi huyo inasemekana aliwafuata watoto hao hadi nyumbani kwa Wazazi wao kila mmoja kwa wakati wake lakini ndani ya muda huo huo.

Alipofika majumbani kwa watoto hao aliwasemelezea kwa wazazi wao kwa kuwataja majina yao kamili.

.Watoto hao waliishi katika eneo la Igogo..

Wazazi walishangaa sana bibi huyo amejuaje majina ya watoto wao na amefikaje nyumbani kwao kwa sababu watoto wakati wanachapwa bakora walisema bibi aliwakuta wakiwa wanachuma maembe na walipomuona walikimbia mbio.

KIFO CHAKE : Bibi Fisi alikufa kwa kuuwawa na watu wanao sadikiwa kuwa majambazi mwaka 2000 akiwa na umri unaokadiriwa 100 na zaidi..On the fateful day MWILI usio kuwa na uhai ( Lifeless body )wa bibi Fisi ulikutwa chumbani kwake ukiwa umekatwakatwa mapanga

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU