VILIVYO HARAMU KWA SABABU YA NJIA ILIYOTUMIKA KUVICHUMA

VILIVYO HARAMU KWA SABABU YA NJIA ILIYOTUMIKA KUVICHUMA

Hizi ni mali ambazo katika asili yake ni halali, lakini uharamu umeingia kwa sababu ya njia zilizotumika kuzipata, njia ambazo zina madhara kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii; vikawa vimeharamishwa kutokana na sababu hiyo. Sababu za kuharamisha miamala ni hizi:
  1. Riba
  2. Ghiliba , kutojua
  3. Dhuluma
  4. kamari na bahatinasibu
Tutazifafanua kama ifuatavyo:

1-  Riba

Allah amemuahidi mwenye kujishughulisha na riba kuwa anaingia vitani na Allah na Mtume wake.
Riba ni ziada iliyoharamishwa kisheria, kwa sababu ina madhara na ina dhuluma.
Riba ina aina niyngi. Maarufu sana na zilizoharamishwa kwa ukali ni hizi: Riba katika mikopo na madeni, na ambayo ni ziada katika mali ya msingi bila ya kuwepo biashara au kubadilishana bidhaa kati ya pande mbili (muuzaji na mnunuzi). Riba hii ni aina mbili:

Riba ya deni:

Hii ni ziada juu ya deni unapofika muda wa kulipa kama mdaiwa hakuweza kulipa.
Mfano wake: (Saidi) alimkopa (Khalid) Dola 1000 ili azilipe baada ya mwezi mmoja. Mwezi ulipokwisha na muda wa kulipa ukawa umewadia, Saidi hakuweza kulipa deni na kutimiza ahadi. Mdeni wake (Khalid) akaweka sharti kwa mdaiwa wake kwamba alipe deni hilo sasa hivi bila ya ziada au alilipe baada ya mwezi mmoja Dola 1100. Akishindwa, basi baada ya miezi miwili atalipa Dola 1200, na mfano wa hivyo.

Riba ya mkopo: 

Maana yake ni kwamba mtu anakopa kwa mtu mwengine au benk kiasi cha fedha kwa sharti kwamba alipe kwa faida watakayo kubaliana kiwango chake, mfano asilimia 5% au chini ya hapo au zaidi ya hapo kila mwaka.
Mfano wake: Ni mtu kutaka kununua nyumba kwa laki moja  na hana fedha za kutosha na, kwa hiyo, akenda benki na kukopa fedha kiasi cha laki moja ili anunue nyumba, kwa sharti la kuilipa benki laki moja na elfu hamsini kwa awamu za kila mwezi kwa kipindi cha miaka matano.
Riba ni haramu na ni miongoni mwa madhambi makubwa madamu tu mkopo una faida, sawa mkopo huo ni kwa lengo la uwekezaji na kuitafutia fedha biashara au kiwanda, au ni kwa lengo la kununua mali muhimu zisizohamishika kama kununua nyumba na viwanja, au ni kwa lengo la kununua vitu vya matumizi ya kawaida vinavyotumika na kumalizika.
Ama kununua bidhaa kwa kulipa kidogo kidogo kwa bei ya juu zaidi kuliko bei yake kwa fedha taslimu hio sio katika riba.
Mfano: Ni mtu anayenunua bidhaa kwa Dola elfu moja kwa fedha taslimu au kwa Dola elfu  na mia mbili kwa malipo ya awamu ya kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja; kila mwezi analipa Dola mia moja kwenye duka linalomiliki bidhaa hiyo. 

Hukumu ya riba

Riba ni haramu iliyoharamishwa vikali sana, kwa ushahidi wa wazi wa Qur’ani na Suna. Ni miongoni mwa madhambi makubwa sana. Hakuna yeyote katika watu wanaofanya madhambi ambaye Allah amemtangazia vita isipokuwa tu mlaji riba na anayeshiriki katika riba. Uharamu wa riba umetajwa katika vitabu vyote vya mbinguni vilivyo tangulia, na sio katika Uislamu tu. Lakini riba imepotoshwa na kupuuzwa katika vitabu hivyo vingine kama zilivyopotoshwa na kupuuzwa sheria nyingine. Allah Mtukufu akifafanua sababu ya kuchukizwa kwake Watuwakitabu na hatimae kuwaadhibu amesema kuwa: «…na kuchukua kwao riba wakati wamekatazwa kuichukua..». (Annisaa, aya 161).

Adhabu ya riba

  1. Mwenye kujihusisha na riba anajitangazia vita kati yake na kati ya Allah na Mtume wake, na kwa hiyo, anakuwa adui wa Allah na Mtume wake. Allah amesema kuwa: «Msipofanya hivyo, mmejitangazia vita na Allah na Mtume wake. Na mkitubu, mtachukua mitaji yenu. Msidhulumu na msidhulumiwe». (Albaqara, aya 279). Hivi ni vita ambavyo vina athari ya kisaikolojia na mwilini. Hali za hofu, mdororo wa uchumi, fazaa na huzuni zinazowapata watu siku hizi hazina tafsiri nyingine isipokuwa kwamba ni matokeo ya vita hii iliyotangazwa dhidi ya anayekaidi amri ya Allah na akala riba au akasaidia mchakato wa riba. Je, ikoje athari ya riba huko Akhera?
  2. Mlaji riba amelaaniwa na ametengwa na rehema za Allah yeye na kila mwenye kumsaidia katika hilo. Imenukuliwa kwa Jabir akisema kuwa: «Mtume wa Allah amemlaani mlaji riba, wakala wake, karani wake na shahidi wake» kisha akasema: «Wote hao ni sawa». (Muslim, Hadithi Na. 1598).
  3. Pia mlaji riba atafufuliwa Siku ya Kiama akiwa katika hali mbaya sana kama mtu mwenye kutetema kutokana na ugonjwa wa kifafa na wazimu. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Wale ambao wanakula riba hawasimami ila kama anavyosimama yule ambaye shetani kamzuga kutokana na kumpagawisha». (Albaqara, aya 275)
  4. Pia mali itokanayo na riba hata kama itakuwa nyingi haina Baraka. Mtu hapati raha, faraja wala utulivu  katika mali hiyo, kama Allah Mtukufu alivyosema kuwa: «Allah huiondolea baraka mali ya riba na huzitia baraka sadaka». (Albaqara, aya 276)
Anayechukua faida za riba iwapo atatubu, anatakiwa achukue msingi wa mali yake na aache kilichobaki.

Madhara ya riba kwa mtu na kwa jamii

Uislamu umekuwa mkali sana katika suala la riba kutokana na athari zake zinazo dhuru mtu mmoja mmoja na jamii kwa jumla. Miongoni mwa athari hizo ni hizi:
  1. Kukosekana kwa uwiano katika ugawaji wa rasilimali na kuzuka kwa tofauti kubwa kati ya matajiri na msikini:
Riba inaiweka mali mikononi mwa kikundi cha watu wachache katika jamii moja, na kuikosesha kundi kubwa la jamii hiyo. Hii ni kasoro katika ugawaji wa mali, pale ambapo kikundi kidogo cha matajiri kinakuwa na utajiri wa kupindukia na waliobaki wanakuwa wavuja jasho, masikini na fukara. Hii ni jamii ambayo inakuwa inakuwa na rutuba ya kuzalisha na kuenea kwa kuchukiana na vitendo vya uhalifu katika jamii.
  1. Mazoea ya ubadhirifu Na kuto weka akiba:
Kurahisisha utoaji wa mikopo kwa faida kumehamasisha wengi kufanya ubadhirifu na kuacha kuweka akiba, kwa sababu mtu anapata wa kumkopesha kila atakapo hitaji. Kwa sababu hiyo, hafikirii hali yake ya sasa na ya baadae, na na anafanya ubadhirifu katika mambo yasiyokuwa ya msingi  mpaka anakuwa na madeni mengi na maisha yanamzonga. Maisha yake yote anabaki kuwa ameelemewa na mzigo wa mikopo na madeni hayo.
  1. Riba ni sababu inayowafanya matajiri kukimbia kuweka vitega uchumi vyenye manufaa kwa nchi:
Mwenye fedha katika mfumo wa riba anapata fursa ya kupata kiwango fulani cha faida kutoka kwenye fedha zake. Jambo hili humfanya aondoke katika kuwekeza fedha zake katika miradi ya viwanda, kilimo na biashara hata kama miradi hiyo itakuwa na faida kubwa kwa jamii, kwa sababu miradi hiyo ya uwekezaji ina kiwango fulani cha  hatari ya uwezekano wa kupata hasara na pia inahitaji aina fulani ya juhudi na kufanya kazi kwa bidii.
  1. Riba ni sababu ya kuondoshwa baraka katika mali na kupatikana kwa mdororo wa kiucumi:
Midororo yote ya kiuchumi na ufilisikaji mkubwa wa mashirika au watu binafsi  ni kwa sababu ya kujikita zaidi katika kujihusisha na riba ambayo ni haramu. Hii ni moja ya athari za kuondoshwa kwa baraka katika mali ambako Allah amekuelezea, tofauti na kutoa sadaka na kuwafanyia hisani  watu; mambo ambayo yanaipa mali baraka na kuifanya iongezeke, kama Allah alivyosema kuwa: «Allah huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka». (Albaqara, aya 276).

Toba ya kuacha riba inakuwaje?

Mwenye kutubu kwa Allah na kabla akiwa ameingia katika mikataba ya riba, ana hali mbili:
  1. Kama yeye ndiye anayechukua faida (mlaji riba), basi atachukua fedha za mtaji wake tu, na hatakiwi kuchukua nyongeza yoyote mara tu baada ya kutubu kwake, kama Allah alivyosema kuwa: «Na mkitubu, mtachukua mitaji yenu. Msidhulumu na msidhulumiwe». (Albaqara, aya 279). 
  2. Kama yeye ndiye anayelipa riba (ziada), basi ana hali mbili:
  • Kama ataweza kuvunja mkataba bila ya madhara makubwa itakuwa wajibu kwake kufanya hivyo
  • Kama hawezi kuvunja mkataba isipokuwa kwa madhara makubwa, atakamilisha mkataba huo huku akitia azma ya kutorudia tena kuingia kwenye mkataba kama huo. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Ambaye yamemfikia mawadha kutoka kwa Mola wake akaacha, atasamehewa yale yaliyopita, na jambao lake litarejea kwa Allah. Na atakaye rudia, basi hao ndio watu wa motoni, wataishi humo milele». (Albaqara, aya 275). 

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU