Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad - Sunnah Ni Kujibu Nini Pindi Unapoambiwa 'Fulani Anakusalimia'?

SWALI:


Katika Miji yetu kuna ada hii: Inaposemwa, “Fulani anakusalimia”, anayesalimiwa hujibu kwa kusema: “Allaah Akusallim" (Akupe amani) wewe na yeye. (Allaahu yusalimuka wa yusalimuhu).


JIBU:

Hii hailingani na Sunnah, bali (mtu anapoletewa salaam kutoka kwa mtu wa mbali, anatakiwa) aseme:

عَلَيْكَ وَعَلَيْهِ السَّلام
"'Alayka wa 'Alayhis Salaam"  (Amani iwe juu yako na juu yake).

Japo (kusema), “Allaah Akusalim wewe na Amsalim yeye” ni du'aa kumuombea yeye usalama na afya, lakini (kujibu),

عَلَيْكَ وَعَلَيْهِ السَّلام
''Alayka wa 'Alayhis Salaam” ndio Sunnah. Na mtu anatakiwa aje na nyiradi zilizo bora (zilizothibiti).

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1