Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad - Mwenye Kunyoa Ndevu Anapata Madhambi


SWALI:

Mwenye kunyoa ndevu zake anapata madhambi kwa kuzinyoa?

JIBU:


Ndio, anapata madhambi. Kwa kuwa kufuga ndevu ni wajibu na kuzinyoa ni haramu. Dalili ya hilo, imekuja katika Sunnah kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth nyingi anaamrisha ndani yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufuga ndevu, kuzirefusha, kuziachia na kuziacha kwa wingi. Matamshi yote haya yamekuja kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na imekuja vilevile jitofautisheni na washirikina na jitofautisheni na majusi. Na imekuja vilevile:

”Allaah Kawalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake. Na wanawake wanaojifananisha na wanaume.”

Na ni jambo linalojulikana kule mwanaume kunyoa ndevu zake, anakuwa amejifananisha na wanawake ambao Allaah Kawaumba bila ya ndevu usoni. Mwenye kufanya hivyo atakuwa anapata madhambi na katumbukia katika maasi, kwa kwenda kwake kinyume na maamrisho na kujifananisha kwake na wanawake.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1