Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad - Kula Chakula Kinachoandaliwa Kwa Ajili Ya Bid’ah Kama Ya Mawlid

Kula Chakula Kinachoandaliwa Kwa Ajili Ya Bid’ah Kama Ya Mawlid

Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad (Hafidhwahu Allaah)


SWALI:

Je, inafaa kula chakula cha watu wa bid’ah kwa kujua kwamba wanaandaa chakula hicho kwa ajili ya bid’ah hiyo, kama kuandaa chakula cha mawlid ya Nabiy?


JIBU:

Ni waajib kuwatanabahisha kwamba wanavuka mipaka katika bid’ah, na kwamba wasifanye yaliyoharamishwa. 

Na mtu hatakiwi kula chakula kinachoandaliwa kwa ajili ya  mambo ya bid’ah na mambo yaliyoharamishwa. 
Kwa hiyo hapasi mtu kutumia chakula hicho bali inampasa atanabahi na atahadhari kuingia katika mambo hayo yaliyoharamishwa.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1