NAMNA YA KUTOA ZAKA YA MIFUGO

Kwanza: Ngamia

Zaka inakuwa wajibu katika aina zote za ngamia, ni sawa wawe na nundu moja au nundu mbili, endapo tu idadi yake itakuwa zaidi ya ngamia watano, kama jedwali ifuatayo inavyo onesha:
Idadi Wajibu wa kutoaIdadi Wajibu wa kutoa
KuanziaMpaka KuanziaMpaka 
59Mbuzi jike mmoja3645Binti labuun
(Ngamia jike mwenye miaka miwili na akaingia wa tatu)
1014Mbuzi jike wawili4660Hikka (Ngamia jike mwenye miaka miwili na akaingia wa nne)
1519Mbuzi jike watatu6175Jidh’a(Ngamia  jike mwenye miaka minne na akaingia wa tano)
2024Mbuzi jike wanne7690Binti labuun wawili (Ngamia jike mwenye miaka miwili na akaingia  wa tatu)
2535Binti Makhadh (Ngamia jike mwenye mwaka mmoja na akaingia  wa pili)91120(Ngamia jike Mwenye miaka mitatu na akaingia wa nne)
Ngamia wakiwa zaidi ya mia na ishirini, wajibu kutoa zaka kwa kila ngamia arubaini ni ngamia jike mmoja ambaye ametimiza miaka miwili na kuingia mwaka wa tatu.  Na katika kila ngamia hamsini atatoa zaka ngamia jike mmoja ambaye ametimiza miaka mitatu na kuingia wa nne. Itafanyika hivyo kwa idadi yoyote itakayo ongezeka.

Pili: Ng`ombe

Zaka ni wajibu katika aina zote za jamii ya ng’ombe, kama vile nyati na wengine ikiwa idadi yake itazidi ng’ombe thalathini, kama ifuatavyo:
Idadi Wajibu wa kutoa
KuanziaMpaka 
3039Ijili (Ng’ombe dume aliyetimiza mwaka mmoja kamili)
4059Musinna (Ng’ombe jike aliyetimiza miaka miwili kamili)
6069Ijili wawili (Kila mmoja awe ametimiza mwaka mmoja kamili)
7079Musinna (Aliyetimiza miaka miwili kamili) + Tabii (Aliyetimiza mwaka mmoja kamili)
80~Ng’ombe wakifika thamanini na zaidi, katika kila ng’ombe 30 atatoa Tabii (aliyetimiza mwaka mmoja kamili), na katika kila ng’ombe arubaini, atatoa Musinna (aliyetimiza miaka miwili kamili).

Tatu: Mbuzi na kondoo

Zaka inakuwa wajibu katika jamii ya mbuzi na kondoo kwa aina zake zote, iwapo idadi yake itazidi arubaini, kama ifuatavyo:
Idadi Wajibu wa kutoa
KuanziaMpaka 
40120Mbuzi jike mmoja
121200Mbuzi jike wawili
201399Mbuzi jike watatu
400~Idadi ya mbuzi au kondoo ikifika 600, zaka yake ni kwamba katika kila mia moja ni mbuzi mmoja = Kwa maana hiyo, katika mbuzi 600 ni mbuzi 6, na katika mbuzi 700 ni mbuzi saba, n.k. 

Nani anapewa zaka?

Uislamu umeainisha maeneo ambayo zaka inatakiwa itumike. Inafaa kwa Muislamu kuiweka zaka katika eneo moja tu au zaidi miongoni mwa maeneo haya, au kuikabidhi kwa taasisi na jumuiya za Kiislamu ambazo itazigawa kwa Waislamu wanaostahiki kupewa. Jambo bora zaidi ni kuigawa zaka ndani ya mji (ambao mtoaji zaka anaishi). 

Makundi yanayostahiki kupewa zaka ni haya yafuatayo:

  1. Fukara na masikini: Hawa ni wale watu ambao hawana kipato kinacho watosheleza katika mahitaji yao ya lazima na ya msingi.
  2. Wanaofanya kazi ya kukusanya zaka na kuigawa. 
  3. Mtumwa ambaye anataka kujikomboa kutoka kwa mmiliki wake. Atasaidiwa na kupewa zaka ili ajikomboe na kuwa huru.
  4. Mtu ambaye ana mzigo wa deni na hawezi kulilipa. Ni sawa deni mtu alilichukua kwa manufaa ya jamii na kulenga kuwafanyia watu jambo jema au kwa manufaa yake binafsi.
  5. Wanaopigania dini ya Allah. Hawa ni wale watu wanaopigana kwa ajili ya kuilinda dini yao na nchi zao. Linaingia katika eneo hili kila jambo ambalo linalenga kuutangaza Uislamu na kulipa nguvu neno la Allah.
  6. Wanaolainishwa nyoyo zao. Hawa ni makafiri ambao wameingia katika Uislamu karibuni, au makafiri ambao kuna matarajio ya kuwa wanaweza kuingia katika Uislamu. Kundi hili halitakiwi kupewa zaka na mtu mmoja mmoja, bali kazi ya kuwapa zaka inatakiwa kufanywa na kiongozi wa Waislamu au taasisi za Kiislamu ambazo zitapima tija  katika kufanya hivyo.
  7. Msafiri mgeni ambaye amekwama na anahitaji fedha. Atapewa zaka hata kama yeye ni tajiri mjini kwake.
Allah akiainisha makundi yanayostahiki kupewa zaka amesema kuwa: «Hakuna vingine isipokuwa kwamba zaka ni ya fukara na masikini na wafanyakazi wa zaka na wanaolainishwa nyoyo zao na watumwa (wanaotaka kujikomboa) na wenye madeni na wanaopigania dini ya Allah na wasafiri». (Sura Attauba, aya 60).

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU