MIAMALA YA KIFEDHA KATIKA UISLAM

MIAMALA YA KIFEDHA

Kila kazi halali ni kazi nzuri ambazo Muislamu anapata thawabu kwa kuzifanya iwapo nia yake itakuwa nzuri. 
Allah ameamrisha kuhangaika katika kutafuta riziki na kulihimiza hilo. Linaonekana wazi hilo katika mambo yafuatayo:
Uislamu umekataza kuomba watu mali madamu mtu anao uwezo wa kufanya kazi na kuchuma kwa juhudi zake na kazi yake. Umeeleza kwamba mtu ambaye anawaomba watu mali ilhali anao uwezo wa kufanya kazi na kuchuma, anapoteza hadhi yake mbele ya Allah na mbele ya watu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mmoja wenu haachi kuwa anaomba mpaka akutane na Allah na ilhali usoni mwake hana chembe ya nyama». (Bukhariy, Hadithi Na. 1405. Muslim, Hadithi Na. 1040).
Mtume swallalahu alayhi wasalam pia amesema kuwa: «Mwenye kupatwa na ufukara  akaushitakia ufukara wake huo kwa watu, ufukara wake   hautamalizwa. Na mwenye kuushitakia ufukara wake kwa  Allah, basi Allah atampelekea haraka ukwasi». (Ahmad, Hadithi Na. 3869. Abuudaud, Hadithi Na. 1645).
Kazi zote za viwandani, za kiutumishi na za uwekezaji ni kazi za heshima zisizokuwa dosari yoyote madamu zipo katika wigo wa mambo ya halali. Katika sheria imethibiti kwamba Mitume walikuwa wakifanya kazi halali ambazo wafuasi wao walikuwa wakifanya, kama alivyosema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kwamba: «Allah hakumtuma Mtume yeyote isipokuwa kwamba alichunga mbuzi na kondoo». (Bukhariy, Hadithi Na. 2143). Nabii Zakaria alikuwa Seremala. (Muslim, Hadithi Na. 2379). Mitume wengine walikuwa wakifanya kazi kama hizo. 
Mwenye kuwa na nia nzuri katika kazi yake akikusuduia kujihudumia yeye mwenyewe na kuihudumia familia yake isiwe tegemezi kwa watu wengine na kuwasaidia wenye shida, atakuwa anapata thawabu kwa kazi yake hiyo, kama alivyosema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kwamba: «Kwa hakika, wewe hutatoa huduma ambayo kwayo unamkusudia Allah isipokuwa kwamba utapewa thawabu kwa huduma hiyo hata tonge ya chakula unayo iweka katika mdomo wa mke wako …». (Bukhariy, Hadithi Na. 56. Muslim, Hadithi Na.1628).

Asili katika miamalati

Msingi katika miamala yote ya kifedha ikiwa ni pamoja biashara, kukodisha na mashirikiano mengine ambayo watu wanashirikiana na kuyahitaji ni kwamba ni halali na yanaofaa, isipokuwa tu mambo machache yaliyo tolewa na ambayo yenyewe ni haramu au yamekuwa haramu kwa sababu ya njia iliyo tumika katika kuyapata.

Mambo ambayo asili yake ni haramu

Haya ni mambo ambayo asili yake Allah ameyaharamisha.Hivyo, Haifa kufanya biashara kwa kutumia mambo hayo, kukodisha au kuzalisha na kuwasambazia watu.
Mifano ya mambo ambayo yenyewe Uislamu umeyaharamisha:  
  • Mbwa na nguruwe
  • Mizoga au sehemu zake
  • Pombe na vileo vyote
  • Dawa za kulevya na kila kinachodhuru afya
  • Zana zinazosambaza uzinzi kwa watu, kama vile mikanda, mitandao na majarida ya ngono.
  • Masanamu na kila kinacho abudiwa badala ya Allah..

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU