KUUTEMBELEA MJI WA MTUME

Mji wa Madina umepata heshima kubwa kwa sababu ya Mtume swallalahu alayhi wasalam kuhama kwenda katika mji huo kiasi kwamba umekuwa bora kuliko maeneo mengine ya dunia baada ya Makka. Kuutembelea mji huu ni jambo la sheria wakati wowote, na halina uhusiano na faradhi ya Hija. Mtume amesema kuwa: (Hakuna kufunga misafara isipokuwa tu kwenda katika misikiti mitatu: Msikiti Mtukufu (wa Makka) na msikiti wangu huu (wa Madina) na Msikiti Aqswaa (uliopo Jerusalem) (Bukhariy, Hadithi Na. 1139. Muslim, Hadithi Na. 1397. Abudaud, Hadithi Na. 2033).

Ubora wa mji wa Madina

Mji wa Madina una ubora mwingi. Miongoni mwake ni:
  1. Kuwepo kwa Msikiti wa Mtume swallalahu alayhi wasalam humo
Mtume alipofika Madina, jambo la kwanza kabisa alilolifanya ni kujenga msikiti ambao baadae ukaja kuwa kituo cha elimu, ulinganiaji (uhubiri) na kusambaza kheri kwa watu. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Swala moja (inayoswaliwa) katika msikiti wangu huu ni bora zaidi kuliko swala elfu moja (zinazoswaliwa) katika msikiti mwingine isipokuwa tu Msikiti Mtukufu (wa Makka)». (Bukhariy 1123. Muslim 1394).
  1. Ni Mji Mtukufu wa amani:
Mtume ameufanya kuwa mji wa amani kwa Wahyi (maelekezo) kutoka kwa Allah. Haitakiwi kumwaga damu humo, kubeba silaha, kumtia hofu mtu, kukata mti na mengine mbali na hayo na ambayo yamo katika uharamu. Mtume amesema kuwa: «Haikatwi miti yake na wanyama pori wake hawakurupushwi na kilichopotea hakiokotwi isipokuwa tu kwa mtu ambaye atakitangaza na haukatwi mti humo isipokuwa tu mtu ambaye anataka kuipa chakula mifugo yake na haitakiwi kubeba silaha humo kwa ajili ya kupigana». (Bukhariy 1736, Abudaud 2035, Ahmad 959).
  1. Baraka katika riziki, matunda na maisha mazuri
Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Ewe Mola wetu, tupe baraka katika matunda yetu na tupe baraka katika mji wetu na tupe baraka katika pishi yetu na tupe baraka katika kibaba chetu. Ewe Mola wetu, kwa yakini Ibrahim ni mja wako na ni kipenzi chako na ni Mtume wako. Na mimi ni mja wako na ni Mtume wako. Yeye alikuomba kwa ajili ya Makka na mimi ninakuomba kwa ajili ya Madina kwa mfano wa yale aliyokuomba kwa ajili ya Makka na mfano wake pamoja nayo». (Muslim 1373).
  1. Allah ameupa kinga ya Tauni (ugonjwa wa kuambukiza) na Dajali (Mpotoshaji)
Mtume amesema kuwa: «Katika njia za kuingilia Madina kuna malaika. Tauni haiingii humo wala Dajali». (Bukhariy 1781, Muslim 1379)
  1.  Ubora wa kukaa, kuishi na kufa humo
Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amemuahidi mwenye kuvumilia ugumu wa mji wa Madina na ugumu wa maisha yake kwamba atapata maombezi yake Siku ya Kiama. Imenukuliwa kwa Saad Bin Abiwaqqaas, Allah amuwiye radhi, akisema kuwa, amesema Mtume kwamba: «Mji wa Madina ni bora kwao lau wangekuwa wanajua. Hakuna yeyote anayeuacha mji huo kwa kuuchukia isipokuwa kwamba Allah anaubadilishia aliye bora zaidi kuliko huyo. Na hakuna yeyote anayevumilia ugumu na shida zake isipokuwa kwamba mimi nitakuwa muombezi wake au shahidi wake Siku ya Kiama». (Muslim 1363)   
Pia amesema Mtume kuwa: «Atakayeweza kufa katika mji wa Madina, basi afe humo, kwa sababu mimi nitamuombea anayekufa humo». (Tirmidhiy 3917, Ibnimaaja 3112)  
  1. Madina ni pango la imani na inasafisha uovu na vitendo vichafu  
Imani inakimbilia Madina hata kama nchi itakuwa na dhiki kiasi gani. Na waovu na wafanyao machafu hawana nafasi humo na hawadumu. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Kwa yakini, imani inajichimbia Madina kama nyoka anavyojichimbia kwenye shimo lake». (Bukhariy 1777, Muslim 147). Pia Mtume amesema kuwa: «Nina apa kwa (Allah) ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake kwamba, hakuna yeyote miongoni mwao anaye ondoka humo kwa kuuchukia isipokuwa kwamba Allah anaweka mbadala humo wa mtu ambaye ni bora zaidi kuliko yeye. Zindukeni! Madina ni kama kinu cha kufua chuma kinachotoa uchafu. Hakitasimama Kiama mpaka mji wa Madina uwasafishe watu wake waovu kama kinu cha kufua chuma kinavyosafisha uchafu wa  chuma». (Muslim 1383) 
  1. Madina inasafisha dhambi
Imenukuliwa kwa Zaid Bin Thabit, Allah amuwiye radhi, akisema kuwa, amesema Mtume wa Allah kwamba: «Kwa yakini mji huo (Yaani Madina» ni mwema, unasafisha dhambi kama moto unavyosafisha uchafu wa fedha». (Muslim 3824)

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU