Kupiga vita itikadi za uzushi katika nafsi:

KUMUAMINI ALLAH

Kupiga vita itikadi za uzushi katika nafsi:

  • Waarabu na mataifa kwa jumla kabla ya Uislamu walikuwa mateka wa ngano, dhana potofu na itikadi za kubuni kiasi kwamba zilienea maeneo yote ya dunia, na hakuna taifa liliosalimika nayo, kiasi kwamba Waarabu, mwanzo, walidhani kuwa Qur’ani ni aina ya ngano au uchawi.
  • Uislamu ulipoleta nuru na muongozo wake uliikomboa akili ikaachana na utawala wa ngano, dhana na itikadi potofu kwa kuweka sheria na misingi iliyolinda akili na roho, na mafungamano yakaelekea kwa Allah pekee na si kwa mwengine. Miongoni mwa sheria na kanuni hizo ni hizi:
  1. Kupiga vita uchawi na ulozi:
Uislamu umeharamisha uchawi na ulozi kwa aina zake zote, na kuufanya kuwa miongoni mwa aina za ushirika na upotevu. Pia umeeleza kuwa mchawi hawezi kufanikiwa si duniani wala akhera, Allah akasema kuwa: «Na mchawi hafanikiwi popote aendapo».  (Sura Twaha, aya 69).
Kama ambavyo umemharamishia Muislamu kwenda kwa wachawi, kuwaomba, kutaka tiba kutoka kwao au dawa. Umetaja kuwa yeyote mwenye kufanya hayo ameyakufuru yale yaliyoteremshwa kwa Mtume swallalahu alayhi wasalam kwa sababu madhara na manufaa yako mkononi mwa Allah pekee, na hakuna anayejua Ghaibu isipokuwa yeye tu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Yeyote aliyekwenda kwa mpigaramli, akamuuliza, akayaamini kuwa ya kweli ayasemayo, basi ameyakufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammad».  (Alhaakim, Hadithi Na. 15)
  1. Manufaa na madhara yako mkononi mwa Allah:
Uislamu umeweka wazi kwamba viumbe vyote, ikiwa ni pamoja na binadamu, miti, mawe na nyota pamoja na kuwa vikubwa, si vingine isipokuwa ni alama zinazotoa ushahidi wa utukufu wa uumbaji wa Allah. Hakuna yeyote anayemiliki nguvu zisizokuwa za kawaida zenye kuleta taathira katika ulimwengu. Ummbaji, amri na uendeshaji wa ulimwengu ni kwa amri ya Allah, kama alivyosema kuwa: «Ee! Ni kwake yeye tu kuumba na kuamrisha. Ametukuka Allah Mola wa walimwengu». (Sura Al-aaraf, aya 54).
Na anayetafakari ukubwa wa viumbe hivyo na ustadi wa uumbwaji wake atajua kwamba Muumbaji wake ni Mola, Mwenye uwezo mkubwa, Muendeshaji mambo ambaye aina zote za ibada zinatakiwa zielekezwe kwake na si kwa mwengine. Yeye ndiye Muumba na visivyokuwa yeye vimeumbwa. Allah amesema kuwa: «Na miongoni mwa alama zake ni usiku na mchana na jua na mwezi. Msilisujudie jua wala mwezi, na msujudieni Allah ambaye amevimumba hivyo ikiwa nyinyi mnamuabudu yeye tu». (Surat Fuswilat, aya 37).
  1. Hakuna ajuaye mambo ya Ghaibu ila Allah pekee
Uislamu umeeleza kwamba hakuna ajuaye Ghaibu na mambo ya baadae ila Allah pekee, na mpigaramli na mchawi yeyote anayedai kuwa anayajua hayo huyo ni muongo, kama Allah alivyosema kuwa: «Na ziko kwake tu funguo za Ghaibu, hakuna azijuaye ila yeye tu». (Sura Al-an’aam, aya 59). Bali kiumbe bora zaidi na mtukufu sana Mtume swallalahu alayhi wasalam amfikishie rehema na amani, hakuwa akimiliki kujiletea yeye mwenyewe madhara wala manufaa, na hajui Ghaibu na mambo ya baadae, sasa vipi iwe aliye chini kuliko yeye ajue? Allah amesema kuwa: «Sema: Similiki kwa nafsi yangu madhara wala manufaa ila yale tu ayatakayo Allah. Na lau kama ningekuwa najua Ghaibu, ningalijizidishia kheri nyingi, na yasingenigusa mambo mabaya. Sikuwa mimi ila tu ni mtoaji maonyo, mtoaji habari njema kwa watu wanaoamini».  (Sura Al-aaraaf, aya 188).
  1. Umeharamishwa mkosi na mtazamo hasi katika Uislam.
Uislamu umeharamisha kuona mkosi kwa vitu, rangi, kauli na mfano wa hayo, na umeamrisha kuwa na matumaini mazuri na kuiangalia hali ya baadae kwa mtazamo chanya.
Mfano wa mkosi kwa ndege ni mtu anayeionea mkosi safari yake iwapo ataona aina fulani ya ndege au akisikia sauti yake mwanzoni mwa safari yake. Na anaweza kuivunja safari hiyo na asiikamilishe. Mtume wa swallalahu alayhi wasalam, ameitaja hali hiyo kuwa ni Shirki, akasema: «Kuona mkosi kwa ndege ni Shirki». (Abudaud, Hadithi Na. 3912. Ibnimaaja, Hadithi Na. 3538), kwa sababu jambo hilo linapingana na imani thabiti ya Muislamu kwamba Allah ndiye Muendeshaji ulimwengu, Mjuzi wa Ghaibu yeye peke yake na si mwenginewe.
Kwa upande wa pili, Uislamu umeamrisha kuwa na matumaini mazuri, kutarajia kheri, kuwa na dhana nzuri kwa Allah na kuchagua matamshi yanayo onesha hivyo. Mtume swallalahu alayhi wasalam, alikuwa «Akipenda kuwa na matumaini mazuri…maneno mazuri». (Bukhariy, Hadithi Na. 5776. Muslim, Hadithi Na. 2224).
Uislamu umeharamisha kuamini mkosi na kutaraji jambo baya kwa kule tu kuona au kusikia aina fulani ya ndege au wanyama.

Matunda ya kuamini kuwa Allah ndiye Mola mlezi:

  1. Imani hiyo inaipa nguvu ari na ushujaa katika moyo, katika kuthubutu na kukabiliana na changamoto, kwa sababu Allah ndiye Muumba, Muendeshaji ulimwengu, Mwenye kufanya atakavyo. Kwa hiyo, Muislamu atamtegemea ili kuzishinda changamoto.    
  2. Kuamini kuwa Allah ni Mola ni kishawishi kikubwa cha kumuabudu Allah, kumpenda na kumtegemea, kama Allah alivyosema kuwa: «Na ni wa Allah pekee (ujuzi wa) Ghaibu ya mbinguni na ardhini, na kwake yeye tu yanarejeshwa mambo yote. Kwa hiyo, muabudu yeye na mtegemee».
  3.  Imani inazisafisha nafsi ziepukane na itikadi za kuzusha. Anayemuamini Allah kiukweli, basi mambo yake yote atayafungamanisha na Allahu pekee. Yeye ndiye Mola wa walimwengu, naye ndiye muabudiwa wa kweli, hakuna muabudiwa wa kweli ila yeye tu. Hatamuogopa kiumbe yoyote, na moyo wake hataufungamanisha na mtu yeyote, na kutokea hapo, atakomboka aondokane na itikadi za kuzusha na dhana.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU