Kuna hekima gani kwenye matendo ya sala?

Dear Brother / Sister,
Maana ya Matendo katika Sala: Kila nguzo na sehemu ya sala ina hekima zake mahususi,
Moja ya majina ya Allah ni al-Hakim (Mwingi wa Hekima). Yaani, kwa hakika anapangilia na kuumba hekima nyingi, mapendefu na malengo ya kila tendo ni Vyake. Ni kweli kwamba kuna maelfu ya hekima katika amri Yake na makatazo yake. Kuna maana nyingi katika kila tendo la sala, ambayo ndio ibada muhimu zaidi.
Tunaweza kuziorodhesha kama ifwatavyo:
Sala ndio nguzo ya dini. Kama tutafikiria kwamba Kaaba ndio nguzo ya ulimwengu, tutafahamu hekima ya kuligeukia Kaaba wakati wa kusali.
Kunyanyua mikono yetu tukiwa tunasema takbir (Allahu akbar) kunamaanisha tunavirusha vitu vya kidunia nyuma yetu na kusimama kusali kwa ajili ya Allah.
Tukisimama kwa miguu yetu, tunawakilisha namna miti inavyoabudu, milima na malaika ambao daima huabudu wakiwa wamesimama.
Tunapoinama, tunaiwakilisha ibada ya wanyama kama ngamia, mbuzi na kondoo namna wanavyoabudu, na malaika mara zote huabudu kwa kuinama.  
Tunaposujudu, tunaiwakilisha ibada ya mnyama anaetambaa, majani na malaika ambao daima huabudu wakiwa wanasujudu.   
Tunapoketi, tunaiwakilisha ibada ya viumbe vyote kwa Allah kwa niaba yetu wenyewe. Mwishowe, tunapotoa salamu upande wa kulia na kushoto, tunautolea salamu ulimwenu mzima.
Isitoshe, tunaposali, tunaufanya mwili wetu na kila kiungo chake kuabudu.
Kusimama na kusoma Quran kwenye sala pia kuna maana. Kuna hekima maalumu kwenye kuinama/kurukuu baada ya kusimama na kusujudu baada ya kurukuu, kunamaanisha kuwa karibu mno na Allah…
Mwanaadamu, akiwa katika hali ya kuiwakilisha ibada kuu inayotekelezwa ulimwenguni kote, anatekeleza kwa Mwingi-wa-Rehema-Mwenye-Kurehemu ibada ambayo inaendelea kuchukua nafasi mwilini mwake pamoja na kuabudu kwa viumbe hai na viumbe tunavyovizingatia kuwa sio hai mara tano kwa siku.
1. KUSIMAMA (QIYAM)
Kwanza, tunasimama, tunanyanyua mikono na kusema Allahu akbar (Allah ndio mkubwa kuliko wote). Hapo, mwanaadamu hurusha nyuma kila kitu isipokuwa Allah na kujielekeza kwa amri Yake na utashi. Utumwa na uja umewekwa hivyo. Hapo, ibada ya viumbe vyote ndio huwakilishwa.  
2. KUINAMA (RUKU)
Baada ya kumsifu Allah kama Anavyostahiki, mwanaadamu hijisikia unyonge kwenye uwepo wa kiburi anachokiinamia kukionesha na kukiinamisha kichwa chake kama ni alama ya heshima na kusema Subhana Rabbiyal-Azim (Utakasifu ni wake Mola Mlezi, Aliye Mkuu). Muumini anaiwakilisha ibada ya viumbe vyote wanaorukuu kwa kufanya hivyo.
3. KUOMBA KWA UNYENYEKEVU (DUA)
Kisha, ananyooka, na kumshukuru na kumsifu Allah kwa sababu Amemwongoza mja kwenye njia iliyonyooka. Kwa muda fulani, anatafakuri, akiwa amesimama, kiburi na utukufu wa Allah na uwepesi na uchache wa tendo lake, kisha anatishiwa.
4. KUSUJUDU (SAJDAH)
Anasujudu na kuweka paji lake la uso chini akijisikia staha na udhaifu kikamilifu na kusema,
‘Subhana Rabbiyal-Ala (Utakasifu ni wa Mola Mlezi, Aliye Mkuu).
5. KUKETI NA KUTOA SALAMU
Baada ya kurudia matendo hayo kwa mpangilio, anajikuta yuko mbele ya Allah pasi na viunganishi vyovyote na kumwomba Yeye msaada.
Vinapokutana viumbe viwili, husalimiana. Katika upande mmoja wa sala (kuketi), anaesali hurudia ibara hizo hizo za salamu ambazo zimetumika kati ya Mtume Muhammad (s.a.w.) na Allah wakati wa safari ya Miraji (kupaa mbinguni):
(Maamkizi mema yote, sala na wema ni wa Allah. Amani iwe juu yako, Ewe Mtume na rehema za Allah na baraka Zake. Amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah!)
Matendo ya mwili katika sala:
Kuna matendo 4 katika sala. Tendo la kwanza ni qiyam, ambalo ni, kusimama. La pili ni ruku (kuinama). La tatu ni sijdah ya kwanza (kusujudu) na la nne ni sijida ya pili. (Fususulhikam,  2/476-477)
Kwenye kisimamo katika sala, kichwa kinamwashiria Mola Mlezi na miguu inawaashiria watu. Mwanaadamu, anayeyachanga matendo yote katika kisimamo, anasoma Quran (qira’ah), ambayo ni fard, katika hatua hii. Anatimiza fard mbili: qiyam na qira’ah.
Kama ilivyo ruku’, inamaanisha kuitenda hali ya wanyama katika sala. Katika hatua hii, miguu ya wanyama inatazama kwenye kitovu cha ardhi, na mwelekeo wa viwiliwili vyao viko kimlalo. Inamaanisha, wanyama husimama sambamba na mvuto wa dunia. Wakiwa wamesimama namna hiyo, kichwa cha mnyama hakitazami eneo wala mvutano wa dunia. Ni hali inayowahusu wao. Kwa nini tunatenda hivyo ilhali sisi ni wanaadamu? Swali kama, ‘Wanyama ni nani kwetu?” linaweza kuibuka. Jawabu ni ifwatavyo: mwili wa mwanaadamu, ambao ni kifupi cha wanyama 18 elfu, una roho ya kinyama inayoishi duniani. Roho hiyo, inayoitwa nafsi kwa upande wa matamanio, haiwezi kupandikizwa kwa binaadamu isipokuwa iwe imesafishwa. Atatakiwa ale kidogo, alale kidogo na ajamiiane kidogo ili awe mbali na upande wa mnyama, ambao ni karibu na dunia. Kisha, atakuwa katika hali ya kusafishwa. Salah (kusali), ambayo ni ibada inayoefahamika, inatakiwa itende uwepo wa mnyama ndani yake.
Hekima ya sajdah; mtu anaposujudu, kichwa kinakwenda chini sawa na kiwango cha miguu. Mtu hutenda hali hii ambayo ni kusujudu kwa mimea.
Kusujudu mara ya pili ni kukosa uhai. Lenyewe halina tendo. Yaani, hakuna tendo linakuja kutoka ndani yake. Inafanya kama ni matokeo ya nguvu kutoka nje. Inayojumuisha mbale ndani ya mawe na sakafu. Mbale inamilikiwa na kitu kinachoitunza isipokuwa ikiyeyushwa kwa kuwa ipo katika hali ya mtawanyiko katika vitu visivyo hai. Elementi ya kila mbale ina roho kwa upande wa atomi zake.
Kusujudu mara ya pili ni kama ya kwanza kwa sababu mimea na vitu visivyo hai viko pamoja; havina matendo kama wanyama. Kila sayari, nyota na vinavyofanana angani havina uhai. Kusujudu ni kukubwa kama kilivyo kiwango chao.
Kwa kuongezea, sala (salah) ni aina ya ibada inayojumuisha mwanaadamu, wanyama na viumbe vyote. Hata hivyo. Inafahamika kwa kutimizwa kimoyomoyo na kiroho na sio kimwonekano.
Maswali juuyau islamu

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1