Kumjua Mtume swallalahu alayhi wasalaam

Ni Muhammad Bin Abdallah Bin Abdulmuttwalib Bin Hashim, Mquraishi. Yeye kwa nasaba ni Muarabu bora sana, swallalahu alayhi wasalam..
1- Kuzaliwa kwake
Alizaliwa Makka mwaka wa 570 Miladiya akiwa yatima wa kufiwa na baba. Alimpoteza mama yake akiwa katika umri mdogo, na hivyo akalelewa katika uangalizi wa babu yake Abdulmutwalib, Halafu baada yake alikuwa katika ulezi wa ami yake Abutwalib ambaye alimhami na kumlinda. 
2- Maisha na kukua kwake
Aliishi katika kabila lake la Kuraishi miaka arobaini kabla ya kupewa utume. Alikuwa mfano bora wa tabia, na alikuwa akipigiwa mfano katika maadili mema na sifa nzuri za kipekee. Jina lake maarufu lilizoeleka lilikuwa Mkweli Muaminifu. Alikuwa akifanya kazi ya uchungaji mifugo halafu akafanya biashara.
 Mtume wa Allah kabla ya Uislamu alikuwa akimuabudu Allah kwa kutumia dini ya Ibrahimu akijitenga na itikadi potofu, na alikuwa akikataa kuabudu masanamu na vitendo vya kishirikina.
3 - Kupewa Utume
Baada ya kuwa Mtume wa Allah,swallalahu alayhi wasalam, ametimiza miaka arubaini katika umri wake, na akiwa anatafakri na kumuabudu Allah katika pango la Hiraa lililopo katika mlima wa Annuur (mmojawapo wa milima ilopo karibu na mji wa Makka), ulimjia Wahyi na Qur’ani kuanza kuteremka. Qur’ani ya mwanzo kabisa kumshukia ilikuwa kauli ya Allah isemayo kuwa: «Soma kwa jina la Mola wako ambaye ameumba». (Sura Al-alaq, aya 1), ili atangaze kwamba utume huu tangu mwanzo wake awamu mpya ya elimu, kusoma, mwangaza na muongozo kwa watu. Halafu Qur’ani iliendelea kumshukia kwa kipindi cha miaka ishirini na tatu.
4 - Mwanzo wa kutangaza dini
Mtume wa Allah alayhi swalatu wasalaam alianza kuitangaza dini ya Allah kwa siri kwa miaka mitatu, halafu akatangaza wazi miaka kumi mingine. Katika miaka hiyo, yeye na Maswahaba wake walikumbana na aina mbali mbali za ukandamizaji na dhulma kutoka kwa kabila lake la Kikuraish. Aliutangaza Uislamu kwa makabila yaliyokuwa yakienda kuhiji. Watu wa Madina waliukubali Uislamu, na waislamu wakaanza kuhama kwenda Madina kidogo kidogo.
5 - Kuhama kwake.
Mtume alihama mwaka (622m) kwenda Madina iliyokuwa ikiitwa Yathrib wakati huo, akiwa na umri wa miaka hamsini na tatu, baada ya mamwinyi wa Kiquraish na waliopinga utangazaji wake dini na kula njama na kutaka kumuua. Aliishi Madina miaka kumi akiutangaza Uislamu; akiamrisha kusali, kutoa zaka na sheria nyingine za Uislamu.
6 - Kutangaza kwake Uislam.
Mtume wa Allah alayhi as’swalatu was salaam aliweka msingi wa mbegu ya ustaarabu wa Kiislamu mjini Madina baada ya kuhama kwake (622-632), na kujenga misingi ya jamii ya Kiislamu. Alifuta ubaguzi wa ukabila, alisambaza elimu na kuweka misingi ya usawa, maadili mema, udugu, ushirikiano na nidhamu. Baadhi ya makabila yalijaribu kuuangamiza Uislamu na, kwa sababu hiyo, yalitokea matukio na vita kadhaa, na Allah aliinusuru dini yake na Mtume wake alayhi swalatu wasalaam. Halafu watu waliendelea kuingia katika Uislamu. Makka na miji mingi, pia makabila mengi katika kisiwa cha Uarabuni yaliingia katika Uislamu kwa hiari, wakiridhishwa na dini hii tukufu.
7- Kufariki kwake
Katika mwezi wa Safar wa mwaka wa 11 tangu Mtume kuhamia Madina na baada ya kuwa Mtume wa Allah amefikisha ujumbe na kufikisha amana, na Allah kuitimiza neema hii kwa watu kwa kuikamilisha dini, Mtume alipata homa na ugonjwa ukamzidia. Alifariki mchana wa siku ya Jumatatu, Mfungosita, mwaka wa 11 Hijiriya (sawa na tarehe 8/6/632m) akiwa ametimiza umri wa miaka sitini na tatu. Alizikwa katika nyumba ya Aisha, ubavuni mwa msikiti wa Mtume,swallalahu alayhi wasalam.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU