Kuamini kwangu kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah kunajumuisha mambo gani?

NINAKIRI KUWA HAKUNA MWENYE KUABUDIWA KWA HAKI ISIPOKUWA ALLAH PEKEE NA MUHAMMAD NI MTUME WAKE

Ni kuamini kuwa habari zake ni za kweli, kutii amri zake, kuyaepuka aliyoyakataza na kumuabudu Allah kwa mujibu wa sheria alizotuwekea Mtume swallalahu alayhi wasalam, na kutufundisha.

Kuamini kwangu kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah kunajumuisha mambo gani?

  1.  Kuamini kuwa habari ambazo amezieleza Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika nyanja zote ni za kweli. Miongoni mwa habari hizo ni:
  • Mambo ya Ghaibu (yasiyo onekana kwa macho), Siku ya Mwisho, Pepo na neema zake na moto na mateso yake.
  • Matukio ya Siku ya Kiyama yatakayo tokea na dalili zake, na matukio yatakayo tokea mwisho wa dunia.
  • Habari za watu wa mwanzo na waliotangulia, na mambo yaliyo tokea kati ya Mitume, Allah awafikishie amani, na kati ya watu wao.
  1. Kutii amri zake na makatazo yake, swalllalahu alayhi wasalam kunajumuisha yafiatayo:
  • Kutii aliyotuamrisha na kuamini kuwa hatamki kutokana na matamanio ya nafsi yake, lakini ni Wahyi utokao kwa Allah,  kama Allah alivyosema kuwa: «Yeyote anayemtii Mtume, kwa yakini amemtii Allah». (Sura Annisaa, aya 80)..
  • Kuyaepuka mambo ya haramu aliyotukataza, ikiwa ni pamoja na tabia mbaya na vitendo vyenye madhara, na kuamini kwetu kwamba sisi kukatazwa mambo hayo ya haramu ni kwa hekima na busara aliyokusudua Allah na ni kwa faida yetu, hata kama wakati mwingine busara hiyo hatuioni.
  • Kuamini kwetu kwamba kutii amri zake na makatazo yake kunatuletea kheri na wema duniani na akhera, kama Allah Mtukufu alivyosema kuwa: «Na mtiini Allah na Mtume ili nyinyi mpate kupewa rehema». (Aal-imran, aya 132).
  • Kuamini kwetu kwamba yeyote anayepinga amri za Mtume,swallalahu alayhi wasalam, anastahiki adhabu iumizayo, kama Allah alivyosema kuwa: «Basi wajihadhari wale wanaopinga amri zake kuwapata fitina (mtihani) au kuwapata adhabu iumizayo». (Sura Annuur, aya 63).
  1. Hatumuabudu Allah isipokuwa tu kwa mujibu wa sheria alizotuwekea Mtume, swallalahu alayhi wasalam. Hilo linajumuisha mambo kadhaa ambayo inapasa kuyasisitiza:
  • Kumuiga: Mwenendo wa Mtume wa Allah,swallalahu alayhi wasalam na miongozo yake, maisha yake kwa yote yaliyomo ikiwa ni pamoja na kauli, vitendo na kunyamazia mambo ni kigezo kwetu katika mambo yote ya maisha yetu. Mja anakuwa karibu na Mola wake na anapanda daraja kwa Mola wake kila anapokuwa anaiga sana mwenendo na muongozo wa Mtume, swallalahu alayhi wasalam. Allah  amesema kuwa: «Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allah, basi nifuateni Allah atakupendeni na kukusameheni dhambi zenu, na Allah ni Msamehevu sana, mwenye kurehemu». (Sura Aal-imraan, aya 31).
  • Sheria ni kamili: Mtume swallalahu alayhi wasalam, ameifikisha dini na sheria zikiwa kamili bila ya kupungua. Haifai kwa yeyote kubuni ibada ambayo Mtume wa Allah, swallalahu alayhi wasalam, hakuiweka kwetu kuwa sheria.
  • Sheria ya Allah inafaa kila wakati na kila mahali: Sheria za dini na sheria ambazo zimekuja katika kitabu cha Allah na mwenendo wa Mtume wa Allah, swallalahu alayhi wasalam, zinafaa kila wakati na kila mahali. Hakuna yeyote anayejua zaidi mambo yenye manufaa kwa watu kuliko yule aliyewaumba na kuwafanya wawepo baada ya kutokuwepo.
  • Kuiga mwenendo wa Mtume: ili ibada zikubalike, ni lazima kuitakasa nia kwa ajili ya Allah na ibada kufanyika kwa mujibu wa sheria alizotuwekea Mtume wa Allah,swallalahu alayhi wasalam, kama Allah alivyosema kuwa: «Basi yeyote aliyekuwa anataraji kukutana na Mola wake, afanye amali ifaayo na asimsishirikishe yeyote katika kumuabudu Mola wake». (Sura Alkahf, aya 110). Maana ya (Ifaayo) ni ya sawa, inayoafikiana na mwenendo wa Mtume, swallalahu alayhi wasalam.
  • Kuharamisha uzushi katika dini: Yeyote aliyezusha kitendo na ibada ambayo haimo katika mafundisho ya Mtume, swallalahu alayhi wasalam amfikishie rehema na amani na akataka kumuabudu Allah kwayo, mfano: Mtu ambaye anabuni sala kwa mtindo usiokuwa ule uliowekwa na sheria, huyo anakuwa amepinga amri yake na anapata dhambi kwa kitendo chake hicho na anarudishiwa mwenyewe, kama Allah alivyosema kuwa: «Basi wajihadhari wale wanaopinga amri zake kuwapata fitina (mtihani) au kuwapata adhabu iumizayo». (Sura Annuur, aya 63). Na Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Yeyote aliyebuni katika jambo letu hili mambo yasiyokuwemo, hayo yatakataliwa». (Bukhari, Hadithi Na. 2550. Muslim, Hadithi Na. 1718).
  1. Kumpenda Mtume,swallalahu alayhi wasalam:
Ni miongoni mwa mambo yanayoambatana na kumuamini Mtume, swallalahu alayhi wasalam, Allah  na Mtume wake kuwa wanapendwa zaidi kwa Muislamu kuliko kitu chochote, kama Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Hawi muumini mmoja wenu mpaka mimi niwe napendwa zaidi kwake kuliko mzazi wake na mtoto na watu wote». (Bukhariy, Hadithi Na. 15. Muslim, Hadithi Na. 44).

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU