JE, DUA INATAKIWA KUWA KWA LUGHA YA KIARABU TU?

JE, DUA INATAKIWA KUWA KWA LUGHA YA KIARABU TU?

Inatakiwa kwa Muislamu kuomba kwa kutumia lugha yake ambayo anaifahamu na kutambua maana yake. Hakika ya Dua maombi ya mja kumuomba Mola wake ambaye anajua siri na yaliyojificha zaidi, na kwake lugha hazitatizi na sauti hazimchanganyi. Muislamu akitaka kuomba kwa kutumia Dua zilizonukuliwa katika Qur’ani na Hadithi basi atazame Dua zilizo karibu zaidi na moyo wake. Anaweza kuhifadhi Dua kwa lugha ya Kiarabu na kujua maana yake au anaweza kuomba kwa maana yake kwa kutumia lugha yake, na jambo hili ni jepesi zaidi.   

Dua zilizonukuliwa

Muislamu anatakiwa kuomba kheri zote za duniani na Akhera atakazo bila ya kuvuka mipaka, kudhulumu na kuonea. Hizi hapa baadhi ya Dua zenye kukusanya mengi ambazo zimenukuliwa katika Qur’ani au Mtume ameomba kwa kutumia Dua hizo. 

Miongoni mwa Dua za Qur’ani

  • «Ewe Mola wetu, tupe mazuri duniani na mazuri Akhera na tukinge adhabu ya moto» (Sura Albaqara, aya 201). 
  • «Ewe Mola wetu, usituchukulie hatua tukisahau au tukikosea» (Sura Albaqara, aya 286). 
  • «Ewe Mola wetu, usizipotoshe nafsi zetu baada ya kuwa umetuongoza, na tupe rehema kutoka kwako. Kwa yakini, wewe tu ndiye mtoaji sana». (Sura Aal-imran, aya 8)
  • «Ewe Mola wetu, tupe kutoka kwa wake zetu na vizazi vyetu burudani ya macho na tufanye viongozi wa wenye kumcha Allah». (Sura Alfurqan, aya 74)  
  • «Ewe Mola wetu, tusamehe sisi na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani, na usiweke katika nyoyo zetu chuki ya kuwachukia wale ambao wameamini» (Sura Alhashri, aya 10)   
  • «Ewe Mola wetu, tumezidhulumu nafsi zetu na usipotusamehe na kuturehemu, bila ya shaka, tutakuwa miongoni mwa wenye hasara» (Sura Al-aaraaf, aya 23).   

Miongoni mwa dua za Mtume swallalahu alayhi wasalam

  • «Ewe mwenye kugeuza nyoyo na macho, ziimarishe nyoyo zetu katika dini yako» (Tirmidhiy 2140, Ahmad 12107)
  • «Ewe Mola wangu, ipe nafsi yangu uchaji wake, na itakase kwa kuwa wewe ni bora wa wenye kuitakasa. Wewe ni Mtawala wake na Mola wake». (Muslim 2722)
  • «Ewe Mola wangu, kwa yakini, katika kheri mimi nakuomba kheri zote; za sasa na za baadae, nizijuazo na nisizozijua. Na katika shari ninakuomba unikinge dhidi ya shari zote; za sasa na za baadae, nizijuazo na nisizozijua». (Ibnimaaja 3846, Ahmad 25137) 
  • «Ewe Mola wangu, kwa yakini, nakuomba unikinge dhidi ya uzembe na uvivu na woga na ukongwe na ubahili. Na nakuomba unikinge dhidi ya adhabu ya kaburini na mtihani wa maisha na mauti». (Bukhariy 6006, Muslim 2706).   
  • «Ewe Mola wangu, nakuomba uongofu na kumuogopa Allah na tabia safi na ukwasi». (Muslim 2721)  
  • «Ewe Mola wangu, nisaidie katika kukutaja na kukushukuru na kukuabudu vizuri». (Abudaud 1522, Nasai 1303) 
  • «Ewe Mola wangu, nisamehe niliyoyafanya na nitakayoyafanya, na niliyoyafanya kwa siri na niliyoyafanya kwa dhahiri, na niliyoyafanya kwa kupitiliza, na ambayo wewe unayajua zaidi kuliko mimi. Wewe tu ndiye utangulizae na wewe tu ndiye uahirishae. Hakuna anayestahiki kuabudiwa ila wewe tu». (Bukhariy 6035, Muslim 771)
  • «Ewe Mola wangu, naomba hifadhi ya ridhaa yako unikinge na hasira zako, na kwa msamaha wako unikinge na adhabu zako, na ninaomba hifadhi kwako. Siwezi kufikia kiwango cha kukusifia kama ulivyojisifia wewe mwenyewe». (Muslim 486)
Mtume amesema kuwa: «Dua kati ya Adhana na Iqama haikataliwi». (Abudaud, 521)

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU