HAKIKA YA DUA

HAKIKA YA DUA

Dua ni hakika ya kuabudu na kuonesha dalili mahususi za kuabudu ambazo ni kukimbilia na kujisalimisha kwa Allah Mtukufu. Allah amesema kuwa: «Na Mola wenu amesema kuwa: Niombeni nitakujibuni. Kwa yakini, wale wanaofanya kiburi cha kuacha kuniabudu (kuniomba) wataingia motoni wakiwa dhalili». (Sura Ghaafir, aya 60)    
Allah Mtukufu ni Mkarimu zaidi ya Wakarimu. Kwa hiyo, mja anapojipeleka kwake hujibu maombi yake na kumpa kwa sababu ya kujinyongesha kwake. Mtume amesema kuwa: «Kwa yakini, Mola wenu ni mwenye haya, mkarimu. Anaona haya mja wake anaponyanyua mikono yake kwake kuirudisha ikiwa sifuri (mitupu)». (Abudaudi 1488 )   

Je, Allah anawajibu wote waombao?

Allah amemuahidi anaye omba kwa njia sahihi bila ya dhuluma au kuwaonea wengine kwamba atamjibu. Amesema kuwa: «Na wanapo kuuliza waja wangu kuhusu mimi, kwa yakini kabisa mimi niko karibu, ninajibu dua ya mwenye kuomba aniombapo». (Sura Albaqara, aya 186)
Lakini kujibu huku kuna aina kadhaa ambazo Mtume amezieleza kwa kusema kuwa: «Hakuna Muislamu yeyote anaye omba dua ambayo haina dhuluma wala kukata udugu isipokuwa kwamba, kwa dua hiyo, Allah atampa mojawapo ya mambo matatu: Ama dua yake itajibiwa haraka na ama Allah atamuwekea akiba kwa ajili ya Akhera ama atamuepusha na jambo baya mfano wa dua aliyo omba». (Ahmad 11133)   
«Enyi waja wangu, lau kama wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binadamu wenu na majini wenu wangekuwa na (mioyo kama) moyo wa mtu muovu sana miongoni mwenu hilo lisengepunguza kitu katika ufalme wangu. Enyi waja wangu, lau kama wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binadamu wenu na majini wenu wangesimama katika uwanja mmoja na kuniomba kisha nikampa kila mmoja alicho omba hilo lisingepunguza katika yale niliyo nayo isipokuwa kama sindano inavyopunguza inapotumbukizwa baharini». (Muslim, 2577)

Taratibu za dua

  1. Kuwa na nia safi (Ikhlas) kwa ajili ya Allah. Dua ni ibada, na kumuomba asiyekuwa Allah ni kumuabudu mwengine badala ya Allah. Allah amesema kuwa: «Yeye tu ndiye aliye hai. Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa ila yeye tu. Kwa hiyo, muombeni yeye mkitakasia yeye tu dini. Sifa njema anazistahiki Allah Mola wa viumbe». Sura Ghaafir, aya 65)  
  2. Muombaji awe na azma thabiti katika kuomba. Hatakiwi kusema: «Akipenda Allah». Anatakiwa awe na yakini ya kujibiwa pamoja na moyo wake kuwa hadhiri. Mtume amesema kuwa: «Mmoja wenu akiomba awe na azma thabiti katika kuomba na kamwe asiseme: «Ewe Mola wangu, ukipenda nipe», kwa sababu hali ilivyo ni kwamba hakuna wa kumlazimisha». (Bukhariy 5979, Muslim 2679)
  3. Kuwa na adabu, unyenyekevu, kujinyongesha pamoja na kutopaza sauti. Allah amesema kuwa: «Muombeni Mola wenu kwa unyenyekevu na kwa sauti ya chini. Kwa yakini, yeye hawapendi wanaovuka mipaka». (Sura Al-aaraaf, aya 55)    
  4. Msisitizo katika kuomba. Ibnimasoud amesema kuwa: «Na Mtume alipokuwa akiomba alikuwa anaomba mara tatu». (Muslim 1794)
  5. Kutokuwa na haraka ya kujibiwa. Mtume amesema kuwa: «Mmoja wenu atajibiwa (dua yake) madamu hana haraka’ akisema: Nimeomba na sikujibiwa». (Bukhariy 5981, Muslim 2735)
  6. Kunyanyua mikono katika kuomba dua. Mtume wa Allah alikuwa akinyanyua mikono yake wakati wa kumuomba  Allah ikiwa ni kuonesha unyonge na unyenyekevu mbele ya Allah.
  7. Kujitakasa na mali ya haramu, kwa sababu hiyo ni mojawapo ya sababu za kutojibiwa kwa dua. Mtume, akimuelezea mtu ambaye ana sababu zote za kujibiwa dua yake lakini chakula chake ni cha haramu, kinywaji chake ni cha haramu na amelelewa kwa vitu vya haramu, amesema kuwa: «Vipi atajibiwa?». (Muslim 1015) Maana ni kwamba jambo hilo la kujibiwa haliwezekani.
Muombaji anapata thawabu kwa kadiri ya unyenyekevu wake kwa Allah.

Miongoni mwa maeneo ya kujibiwa dua

  1. Siku ya Ijumaa: Imenukuliwa kwa Abuhuraira kwamba Mtume wa Allah aliitaja siku ya Ijumaa na kusema kuwa: «Ndani ya siku hiyo kuna muda (ambao) mja Muislamu hatakuwemo katika muda huo akisali na kumuomba Allah Mtukufu jambo isipokuwa kwamba Allah atampa jambo hilo, na (Mtume) alitoa ishara kwa mkono wake akionesha kuwa muda huo ni mchache». (Bukhariy 893, Muslim 853)
  2. Mwisho wa usiku: Mtume amesema kuwa: «Muda wa Mola kuwa karibu zaidi na mja ni ndani ya mwisho wa usiku. Kwa hiyo, ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Allah katika muda huo basi kuwa». (Tirmidhiy 3579, Nasai 572)
  3. Kati ya Adhana na Iqama: Mtume wa Allah amesema kuwa: «Dua kati ya Adhana na Iqama haikataliwi». (Abudaud 521) 
  4. Baada ya swala za Faradhi: Imenukuliwa kwa Abu-umama kwamba, Mtume aliulizwa kuwa: «Ewe Mtume wa Allah, ni Dua gani inasikilizwa zaidi na kukubaliwa? Alijibu kuwa: Ni ndani ya usiku wa mwisho na baada ya swala za faradhi». (Tirmidhiy 3499). Jambo bora zaidi ni kuwa hilo liwe kabla ya Salaam
  5. Katika kusujudu: Mtume wa Allah amesema kuwa: «Muda wa mja kuwa karibu zaidi na Mola wake ni wakati yeye akiwa mwenye kusujudu. Kwa hiyo, ombeni sana». (Muslim 482)  
  6. Katika safari: Imenukuliwa kwa Abuhuraira kwamba, Mtume amesema kuwa: «Dua tatu ni zenye kujibiwa; hazina shaka: Dua ya mwenye kudhulumiwa na Dua ya msafiri na Dua ya mzazi kwa mtoto wake». (Tirmidhiy 1509, Abudaud 1536)
 
Ni wajibu kwa Muislamu kuzikusudia nyakati bora na za uwezekano wa kujibiwa dua.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU