Posts

Donald Trump Aitishia China Kulipa Fidia Kwa Kushindwa Kudhibiti Corona

Image
Rais wa Marekani Donald Trump amesema huenda nchi hiyo ikaitaka China kuilipa fidia kutokana na janga la maambukizi ya Corona kwa kile anachosema kuwa nchi hiyo ilishindwa kuzuia maambukizi ya Corona. Trump amesema kwa sasa uchunguzi dhidi ya China unaendelea wakati huu nchi hiyo ikiwa imeshuhudia zaidi ya vifo vya watu zaidi ya elfu 56. Hivi karibuni Rais Trump alililaumu shirika la Afya Duniani kwa kuegemea zaidi upande wa China. TAZAMA VIDEO II KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE WAKUBWA TU Rais huyo wa Marekani alidai kwamba shirika hilo la kimataifa lilishirikiana na China katika miezi kadhaa iliyopita kupuuza hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona. Rais Trump alisema shirika hilo liliisifu China ingawa pana sababu ya kuwa na mashaka juu ya idadi rasmi iliyotolewa na serikali ya China juu ya vifo vilivyotokana na mambukizi ya virusi vya Corona. Tangu aingie madarakani Rais Trump amekuwa anayatilia mashaka mashirika ya kimataifa na mara kwa mara amekuwa ...

Mgunduzi wa Barakoa Arudi Kazini Baada ya Kustaafu

Image
Mwanasayansi Peter Tsai aligundua Barakoa za N95 mwaka 1992 ambazo alizitengeneza zikiwa na uwezo wa kuzuia virusi kupenya, amerudi kazini baada ya kustaafu ili kugundua namna ya kuzisafisha na kutumika tena. Hii imekuja baada ya uhitaji mkubwa wa barakoa duniani kote kwaaajili ya kujikinga dhidi maambukizi ya virusi vya Corona. TAZAMA  VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE WAKUBWA TU Peter Tsai alistaafu mwaka 2019, lakini tangu janga la Covid 19 lipate kuitikisa dunia, mchango wake umekuwa ukihitajika na amelazimika kurudi kazini. Barakoa za N95 zinazoshauriwa kutumiwa na watumishi wa afya zina ufanisi asilimia 95 kwenye kuchuja, ‘N’ ni kifupi cha ‘Non-resistant to Oil’, huku 95 ikimaanisha ufanisi wake. Mpaka hivi sasa duniani kote visa vya maambukizi ya Corona ni takribani milioni 3 huku vifo vikiwa vimefikia takribani laki mbili.

Askari Wanaswa Wakipokea Rushwa Kuruhusu Malori Kuingia Uganda Bila Kupima Corona, ‘Wanyooshwa’

Image
Jeshi la Polisi nchini Uganda limewakamata na kuwaweka karantini ‘ya selo’ askari walioonekana kwenye kipande cha video iliyochukuliwa eneo la mpaka wa nchi hiyo na Kenya, wakiwaruhusu madereva wa malori kuingina nchini humo bila kupima virusi vya corona; baada ya kupewa rushwa. Mwendesha pikipiki asiyefahamika ndiye aliyerekodi tukio la askari hao waliokuwa mpakani wakipokea mzigo ambao haukuonekana moja kwa moja, lakini waliruhusu lori hilo kupita. Askari hao wamewekwa karantini na wanatarajiwa kupimwa covid-19 kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi. Msemaji wa Wizara ya Afya, Emmanuel Ainebyoona amesema kuwa maafisa hao wawili pia hawakuwa wamevalia mavazi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, kinyume cha maelekezo ya Serikali. TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE WAKUBWA TU “Maafisa hao wawili walionaswa kwenye ile video wamekamatwa. Wamewekwa karantini (kwenye selo tofauti) na watapimwa kama wameathirika na covid-19. Wafanyakazi wote wa mstari wa mbele ...

Korea Kaskazini “Kim Jong Un yuko fiti” Sio Mara ya Kwanza Kwenda Mafichoni

Image
Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba anajua hali ya Kim Joing un , kufuatia madai kuhusu afya ya kiongozi huyo wa Korea Kaskzini. Rais huyo alisema kwamba hawezi kutoa maelezo lakini anatumai kwamba bwana Kim yuko shwari. Kumekuwa na uvumi uliokuwa ukizunguka tangu bwana Kim alipokosa kuhudhuria sherehe za kuadhimisha siku kuu muhimu. Hatahivyo Maafisa wa Korea Kusini wanasema kwamba hakuna lisilo la kawaida nchini Korea Kaskazini. Katika kikao cha faragha siku ya Jumapili waziri anayehusika na maswala ya kuleta amani kati ya mataifa hayo mawili Kim Yeon – chul alisema kwamba serikali ina uwezo wa kiintelijensia kusema kwamba hakuna kisicho cha kawaida kilichokuwa kikifanyika nchini humo. Uvumi kuhusu hali ya kiafya ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini ulianza baada ya kutoonekana katika maadhimisho ya sikukuu ilofanyika tarehe 15 mwezi Aprili. TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE WAKUBWA TU Vyombo vya habari vya Korea Kusini wiki iliopita viliripoti kwam...

Marekani yaionya Iraq kuhusu mashambulizi dhidi ya kambi zake

Image
Marekani yaionya Iraq kuhusu mashambulizi dhidi ya kambi zake Muungwana Blog · Muungwana Blog 2 · 12 hours ago TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, ameionya Iraq akisema nchi yake italipiza kisasi ikiwa kambi za jeshi la Marekani zilizoko Iraq zitashambuliwa tena. Katika mazungumzo ya simu na waziri mkuu wa Iraq Adel Abdel Mahdi, Tangazo la wizara ya mambo ya nje mjini Washington limesema kuwa Pompeo amesisitiza kuwa lazima wanaofanya mashambulizi dhidi ya kambi za Marekani wachukuliwe hatua. Mazungumzo baina ya viongozi hao yalifanyika jana Jumapili, siku moja baada ya wanajeshi watatu wa Marekani kujeruhiwa katika shambulizi la maroketi dhidi ya kambi ya Marekani na washirika wake Kaskazini mwa mjini mkuu wa Iraq, Baghdad, likiwa la pili kubwa kuilenga kambi hiyo katika muda wa wiki moja. Wanajeshi kadhaa wa Iraq pia walijeruhiwa katika shambulio hilo.

UPDATE ZA MAAMBUKIZI YA CORONA 17/3/2020

Image
Update za maambukizi ya Corona Dunia nzima kwa siku ya leo tarehe 17/3/2020, TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE WALIO AMBUKIZA KWA UJUMLA:  182,742 VIFO KWA UJUMLA :  7,174 WALIOPONA KWA UJUMLA:  79,883 NCHI ZILIZO THIBITISHA:  162  COUNTRY, OTHER TOTAL CASES NEW CASES TOTAL DEATHS NEW DEATHS TOTAL RECOVERED ACTIVE CASES SERIOUS, CRITICAL TOT CASES/ 1M POP China 80,881 +21 3,226 +13 68,690 8,965 3,226 56.2 Italy 27,980 2,158 2,749 23,073 1,851 462.8 Iran 14,991 853 4,996 9,142 178.5 Spain 9,942 342 530 9,070 272 212.6 S. Korea 8,320 +84 81 +6 1,401 6,838 59 162.3 Germany 7,272 17 67 7,188 2 86.8 France 6,633 148 12 6,473 400 101.6 USA 4,727 +64 93 +7 74 4,560 12 14.3 Switzerland 2,353 19 4 2,330 271.9 UK 1,543 55 52 1,436 20 22.7 Netherlands 1,413 24 2 1,387 45 82.5 Norway 1,348 3 1 1,344 27 248.7 Sweden 1,121 7 1 1,113 2 111.0 Belgium 1,058 10 1 1,047 33 91.3 Austria 1,018 3 8 1,007 12 113.0 Denmark ...